Connect with us

NBA

VIJANA WANAULIZIA PESA ZAO TU – LEBRON JAMES

$500,000(takribani Bilioni 1.2 za Kitanzania) kwa kila mchezaji kama zawadi baada ya kushinda NBA In-Season Tournament inaweza kuwa sio ishu sana kwa wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa mwenye Timu ya LA Lakers kama MVP LeBron James au Anthony Davis lakini kwa vijana kama Max Christie au Cam Reddish ni fedha ya kubadili maisha yao.

LeBron Jamed wakati anafanya mahojiano baada ya mchezo alisema kuwa

Baada ya kutwaa ubingwa vijana walinifuata na kuniuliza kuwa tunapewa lini fedha zetu? Mi nikawajibu kuwa sifahamu japo kwa kiasi fulani nafahamu lakini sikutaka kuwaambia. Walikuwa na furaha sana.

Katika upande mwingine LeBron hakuacha kuupongeza Uongozi wa NBA kuandaa shindano hili lakini pia hakuacha kutamba.

Haya ni mashindano ya kwanza kabisa. Bila shaka rekodi zitakuja kuvunjwa lakini jambo ambalo halitokuja kuvunjwa ni kuwa sisi ndio mabingwa wa kwanza wa michuano hii na hakuna atakayekuja kuvunja hili na zaidi ya furaha sana kufanya hivyo tukiwa na kundi la vijana wacheshi lakini wachapakazi sana.

LeBron James anakuwa mshindi wa kwanza wa tuzo ya MVP ya NBA In-Season Tournament baada ya kuisadia timu yake kutwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Indiana Pacers kwa vikapu 123-109 kwenye mchezo wa fainali akifunga vikapu 24.

Makala Nyingine

More in NBA