Connect with us

NBC Premier League

SIIFAHAMU SANA KAGERA ILA TUMEJIANDAA KUSHINDA – BENCHIKHA

Makocha wa timu za Simba SC na Kagera Sugar wamezungumza na waandishi wa Habari hii leo kuelekea mchezo wao wa kesho wa ligi kuu ya NBC.

Kocha wa Simba SC, Abdelhak Benchikha alisema

Binafsi sina ufahamu sana juu ya Kagera lakini naambiwa kuwa ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri na washindani lakini na sisi tumejiandaa. Japo ndio kwanza tumerudi kutoka Morocco lakini tumejiandaa vizuri kisaikolojia na kama inavyofahamika kuwa Simba maana yake ni siku zote kuwaza ushindi. Kundi zima lipo tayari kwa mchezo.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime naye alikuwa na haya ya kusema.

Kama ingekuwa ni mimi na kocha tunakimbizana mitaa ya Dar hapa kweli ningemmpoteza lakini kwenye mpira hakuna ugeni isitoshe Simba ina wachezaji wengi wazoefu. Ni timu kubwa inashiriki michuano mikubwa na tunaiheshimu lakini pia tumejiandaa kukabiliana nayo tuibuke na ushindi.

Simba na Kagera Sugar watamenyana kesho kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 10 jioni

Makala Nyingine

More in NBC Premier League