Connect with us

NBC Premier League

GAMONDI: TIMU INACHEZA VIZURI BILA MAWINGA.

Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga akizungumza kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar amewajibu wale wote waliokuwa wakihoji kwanini haanzi na winga kwenye kikosi chake.

Gamondi amesema timu yake ikiwa inacheza na viungo inacheza vizuri zaidi kuliko ikiwa inacheza na mawinga.

Mkitaka nicheze na Mawinga niambieni namtoa nani ili wao wacheze, nimtoe Aziz Ki? Nimtoe Pacome? Nimtoe Clement? Binafsi naamini tunacheza mpira mzuri tukiwa na Viungo kuliko Mawinga.

Miguel Garmondi, Kocha Mkuu wa Yanga.

Miguel Gamondi amekuwa hawatumii mawinga asilia wa klabu hiyo [Jesus Moloko, Denis Nkane, Farid Musa na Wengine] tangu alipojiunga na kikosi cha Yanga mwanzoni mwa msimu huu.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League