Connect with us

NBC Premier League

SIJARIDHISHWA NA SAFU YA USHAMBULIAJI – GAMONDI

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ameonyesha kutoridhishwa kwake na safu yake ya ushambuliaji licha kupata ushindi wa mabao 4-1 kwa kukosa sana magoli hasa kipindi cha kwanza.

Nimefurahi tumepata ushindi huu lakini sijafurahishwa sana na namna tulivyokosa nafasi za wazi za kufunga magoli hasa kipindi cha kwanza. Tumekosa takribani nafasi 6-9 za wazi. Angalau tulistahili kuwa mbele kwa mabao 2-3 kipindi cha kwanza na kurahisisha mchezo mapema.

Kocha Gamondi alisisitiza kuwa hakuna timu nyepesi mnapokuwa mnacheza wote wa ligi moja ni lazima uwe mshindani na mwenye uchu wa kutaka kufunga lakini hali haikuwa hivyo kwa upande wake.

Sio kila siku utapata nafasi zote zile na zipo mechi nyingine unaweza ukapata 1 tu. Tumemiliki mpira vizuri bila shaka lakini bado tuna kazi kubwa sana ya kufanya kwenye suala la umaliziaji na kuzitumia hizi nafasi tunazotengeneza. Tuna michezo mingi ya kimaamuzi mbele yetu na ili ushindi lazima ufunge.

Baada ya ushindi wa leo wa 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama siku ya Jumatano tarehe 20 Disemba 2023 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa

Makala Nyingine

More in NBC Premier League