Connect with us

CAF Champions League

SIMBA YAENDELEA NA KAMPENI YA KUWAITA MASHABIKI UWANJANI.

Klabu ya Simba hii leo imeendelea na kampeni yake ya kuwahamasisha mashabiki kujitokeza katika mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya klabu ya Wydad AC unaotarajiwa kupigwa Jumanne December 19.

Afisa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally amezungumza hii leo na wakazi wa maeneo ya Mbagala akiwahimiza kufika katika mchezo huo huku akiwaonyesha namna Simba ilivyobadilika tangu alipojiunga na kikosi hicho kocha mkuu Abdelhak Benchikha.

“Tulikuwa hatuliridhiki na kiwango cha timu yetu lakini tangu amekuja mwalimu Benchikha tunakwenda mechi ya tatu sasa timu ina mabadiliko makubwa, mmeona namna Simba ilivyokuwa bora. Kilichobaki ni sisi kutoa support yetu ili Simba ishinde.”

“Mwanasimba tukuombe kwamba tarehe 19 Desemba, 2023 tunakuhitaji Uwanja wa Mkapa, kuhakikisha kwamba tunampelekea moto wa volcano mpinzani wetu Wydad. Tujitokeze kwa wingi siku hiyo, hatuna sababu yoyote ya kubaki nyumbani. Usipokuja wewe uwanjani, nani aje?”

“Asanteni sana watu wa Mbagala, mlinambia nikija mtanipiga mawe lakini sasa mmenikaribisha na mmenipa zawadi. Hamna baya.”

  • Ahmed Ally.

Simba hadi hivi sasa inashika nafasi ya mwisho ya msimamo wa Ligi baada ya kuwa na alama mbili [2] ilizozipata baada ya kutoa sare mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Wydad AC wakiwa ugenini.

Simba inauhitaji zaidi huu mchezo ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika kwa msimu huu.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League