Connect with us

International Football

UFAFANUZI FIFA CLUB WORLD CUP 2025

Uongozi wa Shirikisho la soka Duniani, FIFA chini ya Rais wake Gianni Infantino uliketi kikao jijini Jeddah, Saudi Arabia kuelekea nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu 2023, kujadili mambo mbalimbali lakini zaidi ni mfumo wa Mashindano mapya ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025.

Kwa mujibu wa kikao hicho, mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika nchini Marekani na yatahusisha jumla ya vilabu 32 kutoka kwenye kila Bara mwanachama wa FIFA vilivyofanya vizuri kwenye mashindano makuu ya Vilabu kwa kipindi cha miaka minne ya hivi karibuni kuanzia 2020-21 mpaka msimu huu wa 2023-24.

Kwa mabara ambayo ndani ya kipindi hiki kimetoa mabingwa wasiozidi wawili yani kama kulikuwa na mabingwa wawili au mmoja kwa misimu hiyo yote minne basi kutapatikana nafasi za ziada kwa vilabu vingine kushiriki kupitia nafasi zao kwa mujibu wa mifumo rasmi ya ugawaji alama ya bara husika mfano CAF 5 YEAR RANKING SYSTEM kwa Afrika. Izingatiwe kuwa mwaka huu nao unahesabiwa na tayari mabingwa wa misimu iliyopita washakata tiketi ya kushirikia mashindano hayo.

Kwa mfano upande wetu wa CAF ikitokea bingwa wa msimu huu 2023-24 akawa Al Ahly au Wydad AC basi kutakuwa na nafasi nyingine ya kumpata mshiriki mwingine hivyo nafasi 2 zitapatikana lakini bingwa akiwa mwingine basi itabaki nafasi 1 tu kwani tayari zitakuwa timu 3.

Ufuatao ni mtiririko kamili

AFRIKA – JUMLA YA TIMU – 4

Kupitia Njia ya Ligi ya Mabingwa (CAF Champions League) – TIMU 3

1. 2020/21 and 2022-23: Al Ahly SC (EGY)

2. 2021/22: Wydad AC (MAR)

3. 2023/24: ITAJULIKANA MSIMU HUU

4. ITAJULIKANA KUPITIA RANKI

ASIA – JUMLA YA TIMU – 4

Kupitia Njia ya Ligi ya Mabingwa (AFC Champions League) – Timu 3

1. 2021: Al Hilal SFC (KSA)

2. 2022: Urawa Red Diamonds (JPN)

3. 2023/24: ITAJULIKANA MSIMU HUU

4. ITAJULIKANA KUPITIA RANKI

ULAYA – JUMLA YA TIMU – 12

Kupitia Njia ya Ligi ya Mabingwa (UEFA Champions League) – Timu 4

1. 2020/21: Chelsea FC (UINGEREZA)

2. 2021/22: Real Madrid CF (UHISPANIA)

3. 2022/23: Manchester City FC (UINGEREZA)

4. 2023/24: ITAJULIKANA MSIMU HUU

KUPITIA RANKI – TIMU 8

5. FC Bayern München (UJERUMANI)

6. Paris Saint-Germain FC (UFARANSA)

7. FC Internazionale (ITALIA)

8. FC Porto (URENO)

9. SL Benfica (URENO)

10. ITAJULIKANA

11. ITAJULIKANA

12. ITAJULIKANA

KASKAZINI & AMERIKA YA KATI , KARIBIANI – JUMLA YA TIMU – 4

Kupitia Njia ya Ligi ya Mabingwa (Concacaf Champions Cup)

1. 2021: CF Monterrey (MEXICO)

2. 2022: Seattle Sounders FC (USA)

3. 2023: Club León (MEXICO)

4. 2024: ITAJULIKANA

OCEANIA – JUMLA YA TIMU – 1

KUPITIA RANKI

1. Auckland City FC (NEW ZEALAND)

Hii ni kutokana na michuano ya Ligi ya Mabingwa ya OFC -2024 bado hayajachezwa lakini hata hivyo hata zikipigwa hesabu hakuna klabubyoyote inayoiifikia kwa alama timu ya Auckland City.

AMERIKA YA KUSINI – JUMLA YA TIMU – 6

Kupitia Njia ya Ligi ya Mabingwa (CONMEBOL Libertadores) – Timu 4

1. 2021: SE Palmeiras (BRA)

2. 2022: CR Flamengo (BRA)

3. 2023: Fluminense FC (BRA)

4. 2024: TBC

KUPITIA NJIA YA RANKI – TIMU 2

5. ITAJULIKANA

6. ITAJULIKANA

Jumla ya Timu zitakazopatikana hapo ni 31 huku timu 1 ya mwisho ili kuzifanya ziwe 32 itapatikana kutoka kwa Bara ambalo michuano itafanyika lakini taarifa zaidi zitatolewa hivi punde.

Aidha michuano hii itafuata Kalenda ya FIFA na kuhakikisha kuwa haiingiliani na michuano mingine huku pakiwa na mapumziko ya sio chini ya siku 3 kati ya mechi na mechi ili pia kulinda maslahi ya wachezaji ambayo kimsingi ni usalama na afya zao.

Mfumo wa Mashindano haya yatakuwa kama ifuatavyo:

  • Hatua ya makundi ikiwa na makundi 8 yenye timu 4 kila kundi huku ikichezwa mechi moja moja(sio nyumbani na ugenini)
  • Timu 2 vinara wa kila kundi zitafuzu kucheza hatua inayofuata ya raundi ya 16 bora.
  • Utapigwa mchezo mmoja tu kuanzia raundi ya 16 Bora hadi Fainali yani Hakuna Nyumbani na Ugenini.
  • Hakuna play off

Mashindano haya yanatarajiwa kufuata mfumo ule ule wa FIFA World Cup 2022™ na FIFA Women’s World Cup 2023™, isipokuwa tu hapatokuwa na play-off kwa ajili ya mshindi wa 3.

Aidha michuano hii inatarajiwa kufanyika Nchini Marekani(USA) Kuanzia Juni 15 – Julai 13, 2023.

Makala Nyingine

More in International Football