Connect with us

NBC Premier League

MTIBWA SUGAR YAFUFUKIA MANUNGU

Hatimaye Mtibwa Sugar wamepata ushindi wao wa 2 tu msimu huu baada ya kucheza michezo 14 wakiifunga Mashujaa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Wanatamtam hao kutoka Manungu, Turiani walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Seif Abdallah Karihe dakika ya 23 ya mchezo akiendeleza alipoishia baada ya kufunga dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliopita wakifungwa 4-1.

Dakika chache kabla ya mapumziko, Adam Adam aliisawazishia timu yake ya Mashujaa dakika ya 41 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko wakiwa sare.

Kipindi cha pili kilirudi kwa nguvu kwa timu zote mbili lakini Mtibw Sugar walionekana na nguvu zaidi nyumbani. Wakicheza kwa kujiamini na kutafuta matokeo.

Alikuwa ni mshambuliaji kiongozi wa Mtibwa Sugar, Matheo Anthony aliyeihakikishia timu yake kubaki na alama zote 3 nyumbani baada ya kukandamiza msumari wa pili Dakika ya 71. Hili ni goli la 4 kwa Matheo msimu huu.

Ushindi huu unawafanya Mtibwa Sugar kufikisha alama 8 Lakini bado wanaendelea kusalia nyuma ya Mashujaa wenye alama 9 walio nafasi ya 15 huku wao wakiendelea kuburuta mkia lakini angalau kuna kitu kinaonekana kubadilika kwao.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League