Klabu ya Js Kabylie inayoshiriki Ligi kuu nchini Algeria imevunja mkataba na nyota wa kimataifa wa Tanzania Simon Happygod Msuva ambaye alijiunga na klabu hiyo Julai 2023.
Sababu zinazotajwa na vyombo mbalimbali nchini humo ni kutokana na nyota huyo kutokuwa na kiwango cha kuwaridhisha matajiri hao.
Kwasasa nyota huyo raia wa Tanzania, Simon Msuva (30) ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na klabu yoyote kwenye dirisha hili la usajili.
Msuva alijiunga na JS Kabyle akiwa mchezaji huru akitokea Al – Qadisiyah ya Uarabuni. Amewahi pia kuitumikia Yanga, Difaa El Jadidi na Wydad AC.
JS Kabyle ipo nafasi ya nane [8], imecheza michezo kumi [10], na imekusanya alama 14.
Tangu Simon Msuva ajiunge na kikosi cha JS Kabyle amekuwa hapati nafasi ya kuanza mara kwa mara na hajafunga goli lolote kwenye michuano yote akiwa na JS Kabyle