Connect with us

Top Story

MWAMUZI BORA PAPA GASSAMA ATUNDIKA DALUGA.

Mwamuzi bora wa muda wote Barani Afrika Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia leo rasmi ametangaza kustaafu kazi hiyo akiwa na umri wa miaka 44.

Gassama amewahi kuchezesha michuano ya Olympic mwaka 2012, ambapo alikuwa mwamuzi wa mezani katika mchezo wa Mexico dhidi ya Brazil.

Gassama alianza kuwa mwamuzi rasmi mwaka 2007 akichezesha michezo mbalimbali ya Ligi kuu nchini Gambia kwa uwezo mkubwa.

Hadi kufikia kustaafu kwake amechezesha michezo na mashindano yote makubwa yaliyofanyika Barani Afrika ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, kombe la shirikisho na AFCON, na michezo kadhaa ya Kombe la Dunia kuanzia 2014, Brazil hadi 2022, Qatar.

Makala Nyingine

More in Top Story