Connect with us

Top Story

AJALI YA BUS LA TIMU ALGERIA YAUA WATATU.

Klabu ya Mouloufia El Bayadh jana imepata ajali mbaya baada ya gari la timu hiyo kupinduka wakiwa njiani kuelekea katika mji wa Tizi Ouzou kwaajili ya mchezo wa Ligi dhidi ya JS Kabylie uliotarajiwa kupigwa kesho Ijumaa, December 22.

Golikipa wa timu hiyo Zakaria Bouziani, kocha msaidizi Khaled Moffah na dereva wa basi hilo walifariki Dunia. Wachezaji na viongozi wengine walipata majeraha mabaya baada ya ajali hiyo.

Klabu hiyo imetoa taarifa kuwa wengine walioumia hali yao inaendelea vyema.

Shirikisho la soka nchini Algeria limesitisha shughuli zote za michezo nchini humo kwasasa baada ya tukio hilo kutokea hadi pale watakapotangaza tena urejeo wa michezo hiyo.

“Shirikisho la soka nchini Algeria limeamua kusitisha shughuli zote za michezo zilizopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii nchi nzima”.

“Shirikisho pia limeamua kusitisha zoezi la kuchezesha droo ya 32 na 16 bora ya kombe la nchi [Algerian Cup] hadi baadae”.

  • Taarifa kutoka shirikisho la soka nchini Algeria.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amesema amepokea taarifa hii kwa “huzuni na masikitiko makubwa” na kutuma salam zake za pole kwa familia zote zilizoathirika na tatizo hili.

El Bayadh ipo nafasi ya sita [6] ya msimamo wa Ligi kuu kandanda nchini Algeria ikiwa na alama 15 katika michezo 10 iliyocheza ikiwa alama 12 nyuma ya kinara MC Alger.

Makala Nyingine

More in Top Story