Connect with us

AFCON

HESABU KALI KUELEKEA 16 BORA AFCON.

Michuano ya Mataifa Barani Afrika (AFCON) inaendelea kutimua vumbi nchini Ivory Coast ikiwa tayari kila timu imefanikiwa kucheza mechi mbili za mwanzo katika kila kundi.

Dauda Sports tumekuandalia makala na hesabu za kwenye makaratasi kuelekea michezo ya mwisho ambayo itakuwa ni ya tatu katika kila kundi ambayo pia itatoa hatma juu ya timu zipi zitakazopata nafasi kujiunga na timu zingine ambazo tayari zimefuzu katika hatua ya mtoano (16 bora).

KUNDI A.

Baada ya mechi mbili za Kundi A kwa kila timu, ushindani wa pande tatu umeibuka kati ya wenyeji Ivory Coast, Nigeria, na Equatorial Guinea kwa nafasi mbili za kufuzu moja kwa moja.

Guinea ya Ikweta kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi nne, ilipata ushindi wa 4-2 dhidi ya Guinea Bissau Alhamisi, Januari 18. Pia wanashika nafasi ya kwanza dhidi ya Nigeria, ambao pia wana pointi nne baada ya kuifunga Ivory Coast kwa ushindi wa 1-0 katika mechi ya pili. Sare moja itaihakikishia Nigeria kufuzu kwa hatua ya 16 bora. Iwapo Nigeria itaishinda Guinea Bissau na Equatorial Guinea itashindwa kuifunga Ivory Coast, Super Eagles wataongoza Kundi A.

Sare dhidi ya Ivory Coast itaihakikishia Equatorial Guinea kutinga hatua ya 16 bora. Wataongoza Kundi A iwapo watashinda dhidi ya wenyeji nao Nigeria iwapo watashindwa kuifunga Guinea-Bissau. Iwapo Nigeria na Equatorial Guinea zitashinda, timu iliyo na tofauti kubwa ya mabao itamaliza katika nafasi ya kwanza.

KUNDI B.

Cape Verde ilijihakikishia nafasi yake katika hatua ya mtoano kwa kushinda mechi zao mbili za kwanza dhidi ya Ghana na Msumbiji. Mbio za kuwania nafasi ya pili na nafasi ya mwisho ya kufuzu moja kwa moja katika Kundi B inahusisha Misri, Ghana, na Msumbiji.

Wakiwa na pointi sita, Blue Sharks kwa sasa wapo kileleni, wakifuatiwa na Mafarao wenye pointi nne. Katika mchezo wa tatu na wa mwisho katika kundi hili, ushindi kwa Misri utawahakikishia kufuzu, wakati sare inaweza kutosha ikiwa mechi ya Msumbiji na Ghana pia itamalizika kwa sare.

Iwapo Msumbiji au Ghana watapata ushindi, Misri inahitaji angalau sare moja ili kuepuka kushuka hadi nafasi ya tatu, wakiwa bado na nafasi ya kusonga mbele iwapo timu mbili zilizo katika nafasi ya tatu katika makundi mengine hazitalingana na jumla ya pointi zao.

KUNDI C.

Senegal ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kwa kuzifunga Gambia na Cameroon. Vita vya kuwania nafasi ya pili na nafasi ya mwisho ya kufuzu moja kwa moja katika Kundi C inahusisha Cameroon na Guinea.

Simba wa Teranga kwa sasa ipo kileleni ikiwa na pointi sita baada ya kuifunga Cameroon, lakini haina uhakika wa nafasi ya kwanza, huku Guinea ikiwa pointi mbili pekee. Guinea ilisogea hadi nafasi ya pili baada ya kuishinda Gambia. Senegal inahitaji sare pekee dhidi ya Guinea katika mechi yao ya mwisho ya kundi ili kujihakikishia nafasi ya kwanza, wakati matokeo ya sare yataihakikishia Guinea inafuzu kwa 16 bora.

Guinea ina nafasi ya kuongoza kundi iwapo itaifunga Senegal. Indomitable Lions, ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja, bado inaweza kusonga mbele kwa kuwa timu inayoshika nafasi ya pili kwa kuifunga Gambia na kutarajia Guinea kufungwa na Senegal.

KUNDI D.

Katika Kundi D, Angola na Burkina Faso ziko sawa kwa pointi nne, huku Algeria akiwa katika nafasi ya pili akiwa na pointi mbili na Mauritania ikiburuza ikiwa haijafanikiwa kupata pointi hata moja

Algeria watalenga kupata ushindi katika mechi yao ya mwisho ya kundi dhidi ya Mauritania siku ya Jumanne, Januari 23.

Huku wakiwa na matumaini ya matokeo mazuri kati ya Angola au Burkina Faso, mmoja kupoteza ili kujiongezea kuongeza nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.

KUNDI E.

Jumamosi, Januari 20, Mali na Tunisia zilitoka sare ya 1-1, Mali ikiongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, na Tunisia iliyokaa nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja.

Siku iliyofuata Afrika Kusini iliichapa Namibia mabao 4-0 na kupanda hadi nafasi ya pili. Bafana Bafana itafuzu kwa Raundi ya 16 ikiwa itaifunga Tunisia tarehe 24 Januari.

Hali hiyo hiyo inatumika kwa Namibia ambao wanahitaji ushindi dhidi ya Mali mnamo Januari 24 ili kusonga mbele katika hatua ya 16 bora.

Mali wapo katika nafasi nzuri kwani wanachotakiwa kufanya ni kuepuka kichapo dhidi ya Namibia ili wafuzu katika hatua inayofuata. Tunisia, kwa upande mwingine, inaweza kusonga mbele ikiwa tu watawafunga Bafana bila kujali matokeo mengine yatakuaje.

KUNDI F.

Morocco inaongoza msimamo katika Kundi F, lakini sare ya 1-1 dhidi ya DR Congo Jumapili, Januari 21, iliwagharimu pointi muhimu. Simba ya Atlas inafikisha pointi nne, huku DR Congo ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi mbili.

Siku ya Jumapili, Januari 22, Zambia ilipambana na kuizuia Tanzania kwa kulazimisha sare ya 1-1 – na kuziacha timu hizo mbili zikiwa katika nafasi ya tatu, na nne mtawalia kwenye msimamo wa kundi.

Januari 24, Morocco itatinga hatua ya 16 bora iwapo itaepuka kipigo dhidi ya Zambia inayohitaji ushindi ili kutinga hatua inayofuata.

Tanzania inaweza tu kutinga hatua ya mtoano ikiwa itaifunga DR Congo siku hiyo hiyo. Ushindi kwa Congo utawafanya wasonge mbele kwa raundi inayofuata.

Makala Nyingine

More in AFCON