Connect with us

EPL

MAN. CITY NA GIRONA KUTOSHIRIKI UEFA IPO HIVI.

Kwa mujibu wa sheria za UEFA klabu zinazomilikiwa na mtu au kampuni moja kutoka kwenye Ligi mbili tofauti haziwezi kushiriki michuano ya Ulaya [UEFA CHAMPIONS LEAGUE] kwa wakati mmoja, ikitokea zote zimefuzu.

Maswali yamekuwa mengi kwanini RB Leipzing na RB Salzburg zinamilikiwa na kampuni moja na zinashiriki kila mwaka ?.

Jibu: Sheria ya kutokushiriki inakuja pale ambapo tu mtu au kampuni moja linakuwa na hisa kubwa kwenye timu zote mbili, mfano: City Family Group [CFG] wanamiliki hisa asilimia 47, Girona na wao ndio wenye hisa nyingi na 47 Mamchester City wakiwa ndio wenye hisa nyingi.

Kampuni ikiwa na hisa nyingi kuliko wengine inakuwa na nafasi kubwa ya kufanya maamuzi kuliko wenye hisa Chache.

Kwa swala la RB Salzburg na RB Leipzing ni tofauti, Ujerumani wana sheria yao ya umiliki wa 50+1 kwa wanachama na asilimia zingine zilizosalia wanapewa wawekezaji wanagawana.

Hivyo Red Bull hawana nguvu kubwa pale Leipzing, wenye nguvu ni wanachama, hapa ina maana kuwa Leipzing inamilikiwa na wanachama na sio Kampuni.

Red Bull wana nguvu pale Salzburg kwasababu wao wanamiliki takribani asilimia 97 ya hisa za klabu.

Ukitazama umiliki wa timu hizi mbili Salzburg na Leipzing utagundua zinamilikiwa na kampuni mbili tofauti licha ya kuwa na majina yanayofanana, na ndio maana zinashiriki kwa pamoja kwenye michuano ya Ulaya.

Kama ikitokea Girona wamefuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao basi timu zote mbili zinaweza zisishiriki kwasababu ya kuingiliana maslahi kwa maana zote zipo chini ya kampuni moja ya City Football Group.

Janga hili pia linaweza kumkuta Manchester United baada ya Billionaire mpya Bwana Jim Ratcliffe kukamilisha ununuzi wa hisa ndani ya klabu hiyo.

Ikumbukwe Sir Jim anamiliki kampuni ya INEOS ambayo inaimiliki NICE ya Ufaransa kwahiyo Manchester United itakuwa chini ya kampuni ya INEOS akikamilisha kuinunua kitu ambacho kitafanya timu hizi mbili ziwe chini ya umiliki wa kampuni moja.

Ikitokea Manchester United imefuzu UEFA na NICE ikafanikiwa kufuzu pia, timu zote zinaweza zisishiriki kutokana na sheria ya UEFA ya Umiliki wa Klabu.

Makala Nyingine

More in EPL