Connect with us

EPL

REBBECA ATAFUNGUA MILANGO MINGI – KOMPANY

Rebbeca Welch ameweka historia ya kuwa Muamuzi wa kwanza wa Kike kuwahi kuchezesha mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza tangu kuundwa kwake.

Rebbeca mwenye umri wa miaka 40, alichezesha mchezo wa Fulham dhidi ya Burnley, Burnley wakishinda kwa mabao 2-0 kwenye mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Craven Cottage.

Ni uwanja huu huu ambao Rebecca alianza kujumuishwa kwenye michezo ya Ligi Kuu baada ya kuwa muamuzi wa akiba kwenye mchezo ambao Manchester United waliifunga Fulham 1-0.

Rebecca Welch alianza uamuzi mwaka 2010 huku akiwa anafanya pia kazi na NHS kisha akawa muamuzi rasmi mwaka 2019. Itakumbukwa kuwa mwaka 2022 alikuwa miongoni mwa waamuzi waliochaguliwa kuchezesha mechi za FA Raundi ya 3.

Mwaka jana alikuwa sehemu ya waamuzi waliokuwepo na kuchezesha mechi za Kombe la Dunia kwa Wanawake, mashindano yaliyofanyika huko New Zealand.

Baada ya mchezo kumalizika, kocha wa Burnley, Vincent Kompany alisema:

Ni Hatua kubwa kwake na naamini itakuwa ni moja kati ya mechi nyingi zaidi yeye kuchezesha. Kila kitu kinaanza na Mwanzo wake na huu kwake ndio mwanzo wake. Nina furaha sana kwa ajili yake lakini pia kwangu kuwa sehemu ya historia hii.

Rebecca Welch huenda amefungua milango ya waamuzi wengi wa kike nchini Uingereza kuamini kuwa inawezekana kipindi hiki tofauti na walivyokuwa wanafikiria hapo awali.

Makala Nyingine

More in EPL