Connect with us

EPL

TEN HAG AWATOA HOFU MASHABIKI JANUARY WATAKUWA TISHIO.

Kocha mkuu wa kikosi cha Manchester United Erik Ten Hag amesema klabu yake sio miongoni mwa klabu zinazowania kubeba ubingwa msimu huu kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu inayoyapata klabu hiyo hasa baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Westham.

Ten Haag hakuficha hisia zake wakati anazungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa 13 timu hiyo ikipoteza kabla ya Christmass tangu ilipofanya hivyo mwaka 1930 ambapo timu hiyo ilishuka daraja.

“Kwa wakati huu hatupo kwenye ubora, lakini tumeona wiki iliyopita kwenye mchezo dhidi ya timu bora ya hii Ligi kilichotokea”.

“Hatukufunga, tulikuwa na wakati mzuri sana kwenye ule mchezo”.

“Walizuia vizuri sana ndani ya dakika 90, na hivyo ndivyo inatakiwa kiwe kiwango chetu kama tulivyofanya pale. unatakiwa kucheza hivyo kwa kila mchezo”.

Westham United jana ilipata ushindi wa goli 2-0 magoli ya Jarrod Bowen dakika ya 72 na Mohamed Kudus mbele ya Manchester United na kuifanya sasa United izidiwe alama 11 na kinara wa Ligi hiyo Arsenal huku wakiendelea kusalia nafasi ya nane (8) ya msimamo.

Hata hivyo kocha Erik Ten Hag anaamini timu yake itaimarika zaidi baada ya mwaka mpya 2024.

Ten Hag aliongeza kuwa “Mwaka 2023, tulishinda kikombe, tukacheza fainali ya kombe la FA, tukamaliza nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi”.

“Kulikuwa na mambo mengi sana lakini tulikuwa tunacheza vizuri zaidi, lakini kwa kipindi hiki tunacheza vibaha”.

“Kuna sababu ya hilo, tuna majeruhi wengi, kwahiyo timu itakuwa vizuri kama majeruhi watarejea”.

“Tunapaswa kuwa watulivu, tuwe wamoja, kusimama kwenye mipango yetu, tunapaswa kufanya hivyo pamoja”.

Makala Nyingine

More in EPL