New York Knicks leo imeweka rekodi ya kuwa timu iliyocheza michezo mingi zaidi[58] ya ligi ya NBA kwenye sikukuu ya Krismasi na ilinogeshwa zaidi na ushindi dhidi ya Milwaukee Bucks kwa vikapu 129-122.
Alikuwa ni Jalen Brunson aliyekuwa nyota wa mchezo huo akifunga pointi 38 na kushika nafasi ya 3 kwa upande wa New York Knicks kwa waliofunga vikapu vingi siku kama ya leo kwenye chati inayoongozwa na Bernard King aliyefunga pointi 60 kwenye mchezo mmoja aliyekuwa Uwanjani kushuhudia mchezo huo. Alama zingine zilichangia pia na Julius Randle [24], RJ Barret [21] huku Immanule Quickley akiweka rekodi yake ya kufunga alama nyingi zaidi[20] ndani ya muda mchache.
Giannis Anentokounmpo alifunga vikapu 32 Lakini havikuweza kuinusuru timu yake ambayo iliyokuwa kwenye kiwango cha chini hasa kipindi cha kwanza wakiongozwa kwenye robo zote 2.
Hata waliporejea kipindi cha pili, licha ya kukusanya alama nyingi kupitia pia kwa Damian Lillard[32], Khris Middleton[24], Brooke Lopez[14] Lakini kwa baadhi ya wachezaji kama Beasley[0] kutopata hata alama 1 ni moja kati ya siku mbaya sana kazini kwa Bucks leo.
Itakumbukwa mchezo wa mwisho kukutana, Bucka waliwafunga Knicks kwa alama 130-111 huku Middleton na Beasley wakiwa kwenye kiwango Bora sana lakini leo ni kama kisasi kimelipwa huku Knicks wakivunja mwiko wa Bucks wa kutopoteza michezo zaidi ya 5 mfululizo.