Connect with us

Makala Nyingine

CHASAMBI AITEMA YANGA NA PESA NDEFU KISA NAFASI.

Nyota wa klabu ya Mtibwa Sugar Ladack Chasambi amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Simba kwa dau la usajili la Million 70.

Chasambi akiwa Simba atakuwa akipokea kitita cha Million mbili [2] kila mwezi na ameingia mkataba wa miaka mitatu [3] na klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Dar Es Salaam.

Awali klabu ya Yanga pia ilikuwa ikiiwinda saini ya nyota huyo na walikuwa wameweka mezani kitita cha usajili cha Million 70 na mshahara wa million sita [6] kwa mwezi ikiwa ni mara tatu zaidi ya mshahara atakaolipwa Simba.

Sababu ya Ladack kuikataa ofa ya Yanga ni kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho tofauti na klabu ya Simba ambayo inajitafuta.

Klabu zingine zilizokuwa kwenye harakati za kuinasa saini ya mchezaji huyo ni Azam FC ya Dar Es Salaam ambayo ilishindwa vita hiyo kutokana na kuweka dau dogo pamoja na klabu ya AS Vita ya DRC.

Ladack Chasamba ataungana na kikosi cha Simba kuelekea visiwani Zanzibar kwaajili ya michezo ya kombe la Mapinduzi itakayoanza kutimua vumbi hivi karibuni.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine