Connect with us

Boxing

NIGHT OF CHAMPIONS : BOXING ON BOXING DAY NI LEO

Ule usiku uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda masumbwi wengi wa NIGHT OF CHAMPIONS : BOXING ON BOXING DAY hatimae umewadia na ni Leo hii tukishuhudia mapambano makali ya mchezo huu unaovuta hisia za wengi nchini kwa sasa.

Peak Time Promotions ambao ndio mapromota wa Usiku huu wa Mabingwa wamesema kuwa :

Maandalizi yote yapo tayari. Mabondia wote wameshawasili na wamepima uzito tayari hivyo mapambano yote yapo kama yalivyopangwa. Watanzania waje tu kwa wingi, wakate tiketi zao mapema kwani kweli Wanyama wamerudi mjini

Usiku huu unaotarajiwa kuwa na mapambano mengi, Mpambano mkuu unatarajiwa kuwa kati ya Twaha Kassim “Kiduku” wa Tanzania dhidi ya Mohammed Sabyala kutoka Uganda kwenye mchezo usio wa mkanda.

Twaha alisema kuwa ni mpambano wa yeye kurudisha heshima yake baada ya kupoteza mpambano wake dhidi ya Muafrika ya Kusini, Asemahle Wellem.

Watu wangu najua hawakufurahia mimi kupoteza dhidi ya Muafrika ya kusini yule na huu ni mpambano wa kurudisha heshima yangu. Hivyo mashabiki wa Twaha mje kwa wingi muone namna gani bondia wenu nadhamiria kumliza mwaka vizuri

Naye bondia Mohammed Sabyala wa Uganda alisema :

Ndugu zangu watanzania mje mjionee namna gani namfundisha bondia wenu jinsi ya kucheza mchezo wa mapanchi. Siongei mengi.

Mabondia wengine wanaotarajiwa kupanda uliongoni leo ni pamoja na Francis Miyeyusho “Chichi Mawe”, Oscar Richard na wengine wengi. Milango inatarajiwa kuwa wazi kuanzia Saa 10 Kamili huku michezo ikitarajiwa kuanza Saa 12 kamili.

Viingilio vilitangazwa kuwa 10,000 ukikata tiketi mapema lakini utalipia 20,000 kama utanunua mlangoni. VIP ni 30,000 Lakini VVIP Experience(Ring Side) ni 50,000 tu za Kitanzania.

Makala Nyingine

More in Boxing