Connect with us

Boxing

TWAHA KIDUKU AMNYUKA SABYALA

Bondia Twaha Kassim “Kiduku” Rubaha amefanikiwa kumpiga mpinzani wake Mohammed Sabyala kutoka nchini Uganda na kuutetea mkanda wake wa PST.

Twaha, alifanikiwa kushinda kwa pointi huku majaji wote watatu wakikubalina (Unanimous Decision), Jaji Namba 1 – Aga Peter akitoa alama (99-91), Jaji Namba 2 – Pembe Ndava(98-92) na Jaji Namba 3 -Kurwa Makaranga alitoa alama (99-91). Twaha akiwa na alama(99,98,99) na Mohammed Sabyala akiwa na alama (91,92,91).

Kiufundi mpambano ulikuwa mzuri sana na wa kimbinu. Kila Bondia akicheza akijilinda sana lakini hata ngumi hazikuwa nyingi. Zipo nyakati ambazo mabondia wote walionyesha nia ya kutaka kushinda kwa KO lakini umakini wao uliwafanya kufika hadi hizo raundi 10.

Makala Nyingine

More in Boxing