Connect with us

Taifa Stars

MECHI YA BURUDANI NA AMANI, YAPIGWA AMAAN

Mchezo mzuri kuutizama ukiachilia mbali udugu ila ubora wa wachezaji wa timu zote mbili ulifanya mechi ionekane yenye ushindani mkubwa hasa kwenye eneo la kiungo palipojaa mafundi wengi sana wa kabumbu.

Zanzibar Heroes chini ya kocha Hemed Moroco walikuwa na wachezaji wengi wanaofahamika hasa wakiwa wamecheza kwenye vilabu vikubwa Bara. Mudathir Yahya, Hassan Nassor Maulid na Nahodha Feisal Salum walinogesha marashi ya Unguja kwenye eneo la kiungo kwenye mfumo wa 4-3-3 huku Maabad Maabad na Seif Karihe wakiongoza kuleta Shida kwenye safu ya ulinzi ya Kilimanjaro Stars iliyokuwa na sura ngeni nyingi.

Kilimanjaro Stars nayo haikuwa kinyonge eneo hilo, Yusuph Kagoma alitamba sana eneo hilo akiwa na Adolf Bitegeko na Ladaki Chasambi. Wote wakionekana kwenye umbo la 4-3-3 pengine palifanya mchezo uwe wenyebuwiano sawa. Licha ya pilika kadhaa za Simon Msuva na Twariq Yussuf Kumpa sapoti Said Hamis Jr. Lakini milango bado ikwa migumu.

Mpaka mapumziko timu zote zilienda suluhu ya 0-0.

Kipindi cha pili kilirejea kwenye mfumo mfanano na wa kipindi cha kwanza, licha ya mabadiliko kadhaa lakini bado ilionekana mechi iliyojaa zaidi ufundi wa kumiliki mpira na kupiga pasi nyingi. Burudani iliyoje.

ijapokuwa paliongezeka kasi lakini pia paliongezeka umakini na utulivu. Kila mwalimu alikuwa akiridhika na alichokuwa akikiona.

Kuingia kwa Kibu Denis na Sopu paliongeza kasi kidogo eneo la ushambuliaji la Kili Stars na almanusura watumbukize mpira kimiani kupitia Sopu lakini alikosa utulivu.

Mpaka dakika zote 90 zinatamatika, sio Zanzibar Heroes sio Kilimanjaro Stars walioona goli la mwenzake.

Makala Nyingine

More in Taifa Stars