Connect with us

Mapinduzi Cup

MLANDEGE KUFUNGUA PAZIA NA AZAM MAPINDUZI LEO

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Mlandege FC leo wanatarajiwa kushuka dimbani kwenye mchezo wa Ufunguzi wa michuano hiyo dhidi ya Azam FC.

Mlandege wakiwa na sura nyingi ngeni akiwem mlinda lango Athuman Hassan, Emmanuel Masenza, Abdallah Iddy, Optatus Lupekenya na Raphael Charles wanatarajiwa kutoa upinzani mkubwa dhidi ya Mabingwa mara nyingi zaidi wa michuano hiyo.

Azam FC nao wanatarajiwa kuwa na sura ngeni hasa za Vijana kutoka akademia yao wakishirikiana na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza. Wachezaji waliojumuishwa kutoka vijana ni pamoja na David Chiwalanga, Ashraf Kibeku, Ally Mohamed, Ismail Omary, Mahamoud Haji, George William na Pius Severin.

Mechi hii inatarajiwa kupigwa majira ya saa 10.15 jioni kwenye uwanja wa New Amaan Complex.

Makala Nyingine

More in Mapinduzi Cup