Connect with us

EPL

POCHETTINO AKOSHWA NA MADUEKE.

Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino alimsifu Noni Madueke baada ya winga huyo kupiga penati na kuiwezesha timu hiyo na kupata ushindi muhimu Jumatano.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifunga kwa penati dakika ya 89 na kuwashinda Crystal Palace katika uwanja wa Stamford Bridge.

Pochettino, ambaye alikuwa akimkosoa Madueke hivi karibuni, alifurahishwa na kiwango cha mchezaji wake.

Tofauti ni kwamba alifanya kile tulichohitaji. Nimeipenda kwa sababu alionyesha kunikera. Alisikitishwa na mimi kwa sababu hakucheza sana, pia kwa sababu alikuwa majeruhi.

Alisema Pochettino.

Muargentina huyo atafurahi kuona usimamizi wake kwa wachezaji wake ukileta maendeleo chanya kwa haraka. Ni wiki moja tu tangu Pochettino alipotoa tathmini ya uwazi ya ujio wa mchezaji huyo mwezi Januari wa pauni milioni 28.5 ($37m), akitoa wito kwa mchezaji huyo kuboresha kiwango chake.

Kwa kiwango alichokionesha dhidi ya Crystal Palace Pochettino anasubiri kuona ni jukumu gani atakalompa Madueke wakati Chelsea itakapofunga safari fupi kuelekea Kenilworth Road siku ya Jumamosi watakapomenyana na Luton Town.

Makala Nyingine

More in EPL