Connect with us

Mapinduzi Cup

SINGIDA FG NI DHAIFU MBELE YA JKU.

Michezo ya mapinduzi cup inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Mchezo wa mapema zaidi utapigwa majira ya saa 10:15 Jioni na utaihusisha klabu ya KVZ [Zanzibar] dhidi ya Jamhuri [Zanzibar].

Timu hizi mbili zote zinashiriki Ligi kuu ya visiwani Zanzibar, hadi hivi sasa KVZ imecheza michezo 14 ikiwa nafasi ya nne [4] na alama 26, huku Jamhuri ikiwa imecheza michezo 15, imekusanya alama 15 katika nafasi ya 13 ya msimamo wa Ligi hiyo yenye timu 16.

KVZ kwenye Ligi imefunga magoli 20 na kuruhusu magoli 13 hadi hivi sasa, ikiwa imepoteza michezo minne [4], sare michezo miwili [2] na ushindi michezo nane [8].

Jamhuri hadi hivi sasa kwenye Ligi imefunga magoli kumi [10] na kuruhusu kufungwa magoli 18, imepoteza michezo sita [6], sare michezo sita [6] na ushindi michezo mitatu [3].

Mchezo mwingine unaotarajiwa kupigwa majira ya saa mbili [20:15] usiku utazikutanisha klabu za JKU [Zanzibar] dhidi ya Singida Fountain Gate [Tanzania Bara].

Singida msimu uliopita ilicheza fainali na kupoteza dhidi ya klabu ya Mlandege ya Zanzibar, pengine msimu huu wakaendelea pale walipoishia.

JKU hadi hivi sasa kwenye msimamo wa Ligi yao ya Zanzibar wapo nafasi ya kwanza, ikiwa imecheza michezo 15 na kukusanya alama 36.

JKU imefunga magoli 21 na kuruhusu magoli tisa [9], imepoteza mchezo mmoja [1], imetoa sare michezo mitatu [3], na imeshinda michezo 11.

Singida Fountain Gate hadi hivi sasa ipo nafasi ya tano [5] ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 20, imecheza michezo 14 hadi hivi sasa.

Singida Fountain Gate imepoteza michezo minne [4], sare tano [5], na ikishinda mara tano [5], imefunga magoli 17 na kuruhusu magoli 16, Singida inaudhaifu kwenye safu yake ya ulinzi.

Kwenye mchezo huu JKU inaingia ikiwa na ubora mkubwa kwenye eneo lao la ushambuliaji huku Singida Fountain Gate ikiwa dhaifu kwenye eneo lake la Ulinzi.

Baada ya michezo mitatu bila ushindi kwenye uwanja wa Amaan leo panapo majaaliwa tutashuhudia goli la kwanza likifungwa hapa.

Makala Nyingine

More in Mapinduzi Cup