Connect with us

AFCON

ENYEAMA AKANUSHA TAARIFA ZA KUJIUNGA NA TIMU YA NIGERIA.

Taarifa kutoka nchini Nigeria zimekuwa zikimhusisha nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria Vicent Enyeama kurejea kwenye kikosi cha timu hiyo kama kocha wa magolikipa.

Enyeama mwenyewe amesema kuwa hakuna maongezi yoyote yaliyofanyika kati yake na mamlaka za soka nchini Nigeria ili kuchukua nafasi hiyo.

Sijapokea mwito wowote kutoka shirikisho la soka Nigeria [NFF], na hakuna maongezi yoyote yaliyofanyika kuhusu hilo.

Nilichokisema mwanzo ilikuwa ni maamuzi yangu binafsi, nikionyesha nia yangu ya kuitembelea timu kambini wakati wa AFCON.

Nikienda huko, nitaenda kwaajili ya kuwahamasisha vijana ili wapambane.

Vicent Enyeama, Mlinda lango wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria.

Enyeama ni moja ya magolikipa bora waliowahi kuitumikia timu ya Taifa ya Nigeria kwa kiwango kikubwa na anatajwa kuwa golikipa bora wa muda wote Barani Afrika.

Enyeama amewahi kutwaa kombe la Ligi ya mabingwa Barani Afrika mara mbili akiwa na kikosi cha Enyimba cha nchini Nigeria lakini pia akitumika kwenye klabu kadhaa ikiwemo Lille ya nchini Ufaransa, na Maccabi Tel Aviv.

Makala Nyingine

More in AFCON