Ligi kuu ya soka la wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi majira ya saa 10:00 Jioni. Mchezo huo utawakutanisha watani wa Jadi, Simba Queens dhidi ya Yanga Princess.
Hadi hivi sasa klabu ya Simba ipo nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi ikiwa imekusanya alama sita [6] katika michezo miwili iliyocheza, huku ikifunga magoli kumi [10] na kuruhusu magoli mawili [2].
Yanga Princess ipo nafasi ya tatu [3] ya msimamo wa Ligi hiyo ikiwa na alama sita [6] ikicheza michezo miwili [2] na kushinda yote, hadi hivi sasa imefunga magoli nane [8] na imeruhusu kufungwa goli moja [1] pekee..
Leo zinaenda kukutana timu mbili ambazo zote zinasafu bora ya ushambuliaji, na hii inakuwa mechi ya pili kwa msimu huu timu hizi mbili kukutana baada ya kukutana mara ya kwanza mwanzoni mwa msimu kwenye mchezo wa ngao ya hisani uliomalizika kwa suluhu na mikwaju ya Penalty ikaipeleka Simba Fainali.
Kuelekea mchezo huo wa leo, kocha msaidizi wa klabu ya Simba Mussa Mgosi amesema kila timu inahitaji kupata alama tatu katika mchezo huo na timu itakayojichanganya inaweza kupata kipigo kizito lakini timu yake ameiandaa vyema.
Sisi tunajiandaa kupata alama tatu na Yanga pia wamejiandaa kupata alama tatu, goli moja ni pointi tatu, goli mbili pointi tatu, ila akiingia kwenye mfumo zitafika hata 15 na sisi tukiingia kwenye mfumo zitafika 15 mwisho wa siku tunatafuta alama tatu na akiingia kwenye mfumo magoli yatapatikana.
Simba imejipanga vizuri kurudisha heshima yake, kwasababu ilikuwa mabingwa mfululizo mara tatu mara nne imekosa, imekosa kwa tofauti gani kitu ambacho kimefanyiwa kazi, walimu waliokuwepo wamefanya ripoti yao na sisi tumekuja tumefanya ripoti yetu,… kuna mabadiliko mengi sana kwenye swala la wachezaji lakini pia katika benchi.
Ligi ni ngumu kila timu ina malengo yake, na wanajipambanua kufika kwenye malengo ambayo wamejipangia, mechi ya Simba na Yanga inaonyesha taswira ya soka la wanawake limepiga hatua kiasi gani.
Mussa Hassan mgosi, Kocha Msaidizi Simba Queens.
Nahodha wa kikosi cha Simba Queens Violeth Nicolaus akizungumza kwa niaba ya wachezaji amesema wachezaji wote wamejipanga vizuri ili kuitetea klabu yao ya Simba Queens mbele ya Yanga Princess.
Mchezo wa Derby haujawahi kuwa mrahisi hata timu iwe vipi, wachezaji tumejiandaa vizuri kwaajili ya mechi ya leo ili uweze kutimiza malengo yetu tuliyojipangia ili kuitetea Simba yetu.
Mechi ya leo itakuwa nzuri kwasababu kiufundi,kitimu, timu zote zimejiandaa vizuri katika msimu huu, mechi itakuwa ya ushindani kwahiyo tunaomba mashabiki, wapenzi wa mpira leo waje kuona Burudani.
Violeth Nicolaus, Nahodha wa kikosi cha Simba Queens.
Kwa upande wa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Princess Charles Haalubono amesema anawajua wachezaji wa Simba Queens kwani amewaona katika mchezo wa ngao ya jamii lakini kuhusu ushindi amesema ni kitu kinachotengenezwa kutokana na maandalizi mazuri.
Kila mechi inakuwa tofauti, hauwezi kutarajia kitu kilekile kilichotokea kwenye mechi iliyopita, hii itakuwa mechi ya tofauti lakini tumecheza nao katika mchezo wa ngao ya jamii, nimewaona wachezaji wao,
Kwangu mimi kila mechi inahofu yake, hauwezi kuingia kwenye mechi ukasema huna hofu hata timu ndongo inaweza kukushangaza, kwahiyo kuna hofu kwa kila mechi lakini mhimu ni kuipunguza hiyo hofu.
Ushindi unakuja kutokana na maandalizi, unajiandaa vizuri, unaweka kilakitu kwenye mstari, kila kitu kitaenda kuwa sawa.
Charles Haalubono, Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Princess.
Kwa upande wa wachezaji kupitia kwa nyota wa kikosi cha Yanga princess Saiki Atinuke amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba.
Tumefanya kazi kubwa sana kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa leo, kila mchezaji amefata maelekezo ya mwalimu nafikiri mchezo utakuwa rahisi kwa upande wetu.
Saiki Atinuke, Mchezaji Yanga Princess.
Waamuzi wa mchezo huo wa leo Tatu Malogo [Mwamuzi wa kati] – nTanga, Zawadi Yusuph [Mwamuzi Msaidizi 1] – Tanga, Fatuma Mambo [mwamuzi msaidizi 2] – Iringa, Ester Tagale [Mwamuzi wa akiba] – Dar Es Salaam, Khadija Mastoka [Kamishna wa mchezo] – Dar Es Salaam.
Ligi kuu soka Wanawake Tanzania Bara kwasasa naongozwa na klabu ya JKT Queens iliyocheza michezo mitatu [3] ikavuna alama tisa [9], ikifunga magoli 15 na haijaruhusu nyavu zake kutikiswa hadi hivi sasa.
Makala Nyingine
-
Makala Nyingine
/ 10 months agoUWANJA WENYE HISTORIA YA PELE NA MARADONA KUFUNGUA WORLD CUP.
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza rasmi tarehe ya ufunguzi wa fainali za kombe...
By Lamarcedro -
Tetesi za usajili
/ 12 months agoCHAMA KUONDOKA SIMBA JUNE 2024.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chotta Chama mkataba wake...
By Lamarcedro -
Makala Nyingine
/ 7 months agoZEROBRAINER0 : NA DUNIA YAKE YA MITANDAO YA KIJAMII
Kwenye Vitabu vya Historia ya wachezaji nguli kweli kweli waliowahi Kutamba na Mtibwa Sugar...
-
-
CAF Champions League
/ 7 months agoNI ESPERANCE V AL AHLY CAF CHAMPIONS LEAGUE
Esperance Watakuwa wenyeji wa Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali ya Ligi...
-
Azam Sports Federation
/ 8 months agoHII HAPA RATIBA CBFC ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI
Droo ya Kombe la CBFC(CRDB BANK FEDERATION CUP) 2024 Hatua ya Robo Fainali imechezeshwa...