Connect with us

AFCON

NIGERIA YAMTEMA NDIDI YAMUONGEZA ALHASSAN AFCON 2023.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Super Eagles [Timu ya Taifa ya Nigeria] Jose Peseiro amemuongeza kikosini kiungo wa klabu ya Royal Antwerp inayoshiriki Ligi kuu nchini Ubelgiji Alhassan Yusuf kwaajili ya michuano ya AFCON 2023 inayotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast siku chache zijazo.

Alhassan anachukua nafasi ya kiungo wa klabu ya Leicester City inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini England, Wilfred Ndidi ambaye aliumia jana wakati anaitumikia klabu yake ya Leicester City kwenye mchezo wa Ligi daraja la kwanza nchini England.

Nigeria imepangwa kundi A pamoja na mwenyeji Ivory Coast, Equatorial Guinea na Guinea Bissau. Mchezo wa kwanza wa Nigeria utakuwa dhidi ya Equatorial Guinea, January 14, Mchezo wa pili utachezwa dhidi ya Ivory Coast, January 18 [Michezo miwili ya mwanzo itapigwa katika uwanja wa Stade Olympique Alassane Ouattara – Abidjan], mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Guinea Bissau, January 22 [Uwanja wa Stade Felix Houphouet – Abidjan].

Makala Nyingine

More in AFCON