Connect with us

Makala Nyingine

OKRAH KUANZA KAZI RASMI YANGA KESHO VS KVZ.

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Musa Ndaw amesema kesho wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara na wale waliorejea kutoka majeruhi watapata nafasi ya kucheza.

Kesho tutawapa nafasi wachezaji ambao hawajapa muda wa kucheza na waliorejea kutoka majeruhi kama vile Lomalisa, Okrah, Shehan na wachezaji wengi kutoka timu ya vijana.

Mussa Ndaw, Kocha msaidizi Yanga.

Yanga kesho itakuwa na kibarua dhidi ya KVZ, ikiwa ni mchezo wa tatu [3] wa klabu hiyo na wa mwisho kwenye michuano ya mapinduzi inayoendelea hapa viziwani Zanzibar, imeshinda michezo yote miwili ikifunga magoli saba [7] na kuruhusu goli moja [1] pekee.

Kocha mkuu wa KVZ, Ali Muhammad amesema wamejipanga vizuri kupata ushindi kwenye mchezo huo kwakuwa wamepata muda wa kutosha wa kujiandaa (siku nne).

Yanga ndiyo timu niliyoitazama mara nyingi zaidi kuliko timu zote Tanzania, kwahiyo najua nakwenda kukutana na timu bora.

siwezi kutoa password ya mbinu, tunakwenda kutafuta ushindi lakini pia kujilinda , tutacheza kwa nidhamu.

Ali Muhammad, kocha mkuu wa kikosi cha KVZ.

Mshambuliaji kinara wa klabu ya Yanga ambaye tayari ameweka kambani magoli mawili Crispin Ngushi amesema huu ndio wakati wa wachezaji hao kuweka historia vyema kwenye michuano hii ya mapinduzi na hawana mechi ndogo.

Yanga hatuna mashindano madogo, hatuna mechi ndogo na sisi ambao huwa hatupati nafasi, hii ni fursa kwetu kuonesha kitu kwa benchi la ufundi.

Crispin Ngushi, Mshambuliaji Yanga.

Mechi ya Yanga na KVZ itapigwa kesho saa 2:15 usiku katika uwanjwa wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine