Connect with us

NBC Premier League

ANGUKO LA BIKO IHEFU LA SIKITISHA WENGI.

Klabu ya Ihefu inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara yenye maskani yake Mbarali mkoani Mbeya rasmi leo imetangaza kuachana na Afisa Mtendaji wake mkuu Biko Scanda.

Uongozi wa timu yetu ya Ihefu Sc imefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha Mkataba wa kazi na aliekua Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu yetu Ndugu. Biko Mangasini Scanda.

Hata hivyo Uongozi wa timu unamshukuru sana Biko kwa utendaji wake chanya ndani ya timu yetu kwa muda aliokua nasi na bado una thamini na kupongeza kazi alizofanya.

Ihefu Sc inamtakia kila la kheri Ndugu Biko scanda katika Majukumu yake mengine.

Taarifa rasmi kutoka kwenye klabu ya Ihefu.

Biko amedumu kwenye kikosi hicho kwa muda wa siku 42 kutoka November 22, 2023 alipotangazwa rasmi hadi leo wakati taarifa hiyo inatolewa.

Biko Scanda anasifika zaidi kwenye Football Economy, akilenga hasa kukuza uchumi wa klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara.

Wakati wa utambulisho wake wengi waliamini pengine ndio wakati sahihi ambao mtendaji huyo wa kuweza kuonyesha kwa vitendo kile alichokuwa anakizungumza ili ikiwezekana na klabu zingine ziige.

Baada ya taarifa ya kuondoka kwa CEO Biko Scanda kwenye klabu ya Ihefu “Wana Mbogo Maji” maoni ya watanzania na wapenda soka yamekuwa mengi wengi wakiamini imekuwa haraka sana kwa Ihefu kuachana na kiongozi huyo.

Football Economy imegoma kufanya kazi, bora walikuingiza kwenye uadui na Yanga bila sababu.

Mdau mmoja wa soka alisema.

Huwezi kuendelea kuwa kwenye taasisi kama utasimamia ukweli, Scanda sio kinyonge kaka, aoka letu halipendu usimamie ukweli.

Shabiki mwingine alitoa maoni yake.

Kwa upande wa pili, kutokana na maandiko yake kadhaa yaliyokuwa yakizilenga timu kubwa za hapa nchini wengi walikuwa wakimtazama ili waone kama ataweza kufanya kile alichokuwa anakisema, nao walitoa maoni yao.

Football economy chaliiiii unadhan wakina Hers said wanaigiza pale, wale wanajua utendaji wa Kazi kwa vitendo sio wewe maneno mengi vitendo zero.

Mdau mmoja wa soka alichangia.

football economy inafanya kazi kwenye uchambuzi tu au mazingira ya kazi magumu ama ndio anaenda kuchukua nafasi pale yanga.

Mdau mwingine wa pili alichangia.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League