Connect with us

AFCON

KOCHA STARS AOGOPA KUZUNGUMZA KISA MASHABIKI.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Adel Amrouche amesema kuwa kufikia kesho kikosi chote kitakuwa kimewasili kambini nchini Misri.

Nafikiri kufikia kesho wachezaji wote wanaweza kuwa hapa, lakini kila kitu kipo sawa.

Kuna sura nyingi mpya kwenye hii timu, ni nafasi nzuri ya kufahamiana na kila mmoja, na kufanya kazi pamoja, mipango yetu inaenda taratibu taratibu.

Adel Amrouche, Kocha Taifa Stars.

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Misri ikiwa nchini Misri ilipokita kambi kabla ya kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya mashindano.

Kuelekea mchezo huo wa kirafiki jumapili hii, kocha Adel amesema haijalishi ni matokeo ya aina gani atayapata kitu anachozingatia zaidi ni kuona mbinu zake zinafanya kazi.

Misri, Brazil au timu yoyote kwangu mimi ni mechi tu ya kawaida kwani hii mechi sio kwaajili ya kuonyesha watu nani anaenda kushinda, lakini naenda kuangalia wachezaji ambao sikuwa na nafasi ya kuwaona hapo kabla.

Matokeo sio mhimu sana tunaweza kushinda au kupoteza, kitu cha msingi tupo AFCON, tutawajaribu wachezaji kwenye nafasi mbalimbali cha mhimu sio matokeo.

Unajua Misri ni timu kubwa, lakini kwetu sio lengo letu kushindana bali tunawapa wachezaji nafasi nzuri ya maandalizi.

Adel Amrouche aliongeza.

Adel aliita wachezaji 30 waliounda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania lakini kutokana na majukumu ya wachezaji wengine bado hawajawasili kambini hadi hivi sasa akiwemo nahodha Mbwana Samatta.

Kocha Amrouche ana kibarua cha kupunguza nyota wengine watatu kabla ya kuelekea nchini Ivory Coast kwani idadi inayohitajika ni wachezaji 27 pekee.

Kwa upande mwingine kocha Adel ameonyesha hofu kuzungumzia kile kinachoendelea ndani ya kambi hiyo akihofia watu wa nje wasije kumnukuu tofauti.

Sitaki kuzungumzia matatizo ambayo tunayo, kwasababu mara ya mwisho nilifanya makosa kuongelea kilichotokea ndani ya timu.

Sio kuhusu watu wetu lakini watu kutoka nje wanafuata kile tunachozungumza kuhusu timu yetu, kitu pekee ninachoweza kusema ni kwamba tunafanya kile tulichonacho.

Adel Aliongeza.

Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za Zambia, DR Congo na Morocco.

Makala Nyingine

More in AFCON