Connect with us

AFCON

MAJERAHA YAMUONDOA STARS FUNDI WA BOLI AFCON.

Nyota wa Telford United ya Uingereza Twariq Yusuf Kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kuwa hatokuwa sehemu ya Kikosi cha Tanzania kitakachoshiriki AFCON 2023 huko Ivory Coast kufuatia majeraha yanayomkabili.

“Isivyo bahati sitashiriki michuano ya AFCON, Madaktari wamepambana kwa uwezo wao hadi dakika ya mwisho kutibu majeraha niliyonayo, kitakuwa kitu kibaya zaidi kama nikiendelea.

“Timu imefanya kila kitu kwaajili ya timu lakini mwisho imekuwa hivyo.

“Ndo hivyo ilivyotokea na hakuna kitu klabu inaweza kufanya lakini Mungu pekee ndiye anayejua.

“Kocha amenipa matumaini sana, na ninashauku ya kurejea tena, najivunia hii nafasi na nitakuwa natazama na kuisapoti timu nikiwa nyumbani sehemu ambayo nitakuwa nafanya matibabu”.

Twariq alikuwa sehemu ya kikosi cha mwisho ambacho kilitangazwa na tayari kipo kambini misri kwa maandalizi ya Michuano hiyo.

Makala Nyingine

More in AFCON