Makala Nyingine

NAMUNGO KUACHANA NA SHIZA KICHUYA

Published on

Klabu ya Soka ya Namungo inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara, kupitia kwa Mkuu wake wa Idara ya Habari Bwana Namlia Kindamba, imeweka wazi kuachana rasmi na mchezaji wao Shiza Ramadhan Kichuya.

Kindamba amesema kuwa dirisha hili ndogo wanatarajia kufanya mabadiliko kadhaa ya kikosi yatayoendana zaidi na matakwa ya Kocha wao Mpya, Mwinyi Zahera.

Shiza kama ilivyokuwa kwa Lusajo pia alikuja kuomba ruhusa ya kuondoka hivyo akakaa chini na Uongozi na kukubaliana ikiwemo yeye kulipa gharama za kuvunja mkataba ambazo alizilipa. Hivyo niseme wazi kuwa hatokuwa sehemu ya mipango ya Kocha wetu

Katika upande mwingine hakusita kuiainisha Mipango kabambe ya timu hiyo punde tu mashindano mbalimbali yatakaporejea.

Bado hatujatoka kwenye mipango na malengo yetu. Tunatazamia angalau kwenye michuano ya ASFC tufike Fainali yani tutoetoe timu hapa kati lakini kufika fainali ni moja ya mipango yetu.

Aidha alizungumzia pia kuhusu mipango ya usajili ya dirisha hili dogo ili kuziba mapengo yanayoahwa.

Tunaachana na wachezaji wawili muhimu sana kwenye kikosi chetu ambao tungetamani kuendelea nao lakini hatuna budi kuziba nafasi zao. Hivyo lazima tuingie sokoni ili kupata wachezaji wa aina zao. Japo ni kama kamari kipindi hiki kupata wachezaji Bora ambao labda wapo huru. Na lazima ujiulize Kwanini wapo huru. Walio bora wengi wapo na timu zao, hivyo lazima uvunje benki.

Alimaliza Kindamba.

Popular Posts

Exit mobile version