Connect with us

AFCON

TAIFA STARS NDIO TIMU YA VIJANA ZAIDI AFCON.

Kuelekea kwenye michuano ya AFCON timu yetu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kwa mujibu wa ukurasa wa Pharaohs kwenye mtandao wa X (zamani twitter) umeirodhesha Taifa Stars kwenye nafasi ya kwanza kati ya mataifa 24 yanayocheza michuano hiyo kuwa na kikosi chenye umri mdogo zaidi kuliko timu zote zinazocheza AFCON ya mwaka huu nchini Ivory Coast

Taifa Stars ina wastani wa umri wa miaka 24.64 ikifuatiwa na taifa la Equatorial Guinea lenye wastani wa umri wa miaka 24.7

Mbali na mataifa hayo mataifa mengine yaliyongia tano bora ya wenye wastani wa umri mdogo zaidi ni pamoja na taifa la Guinea-Bissau,Cameroon pamoja na Burkina Faso

Kwenye orodha hiyo mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo timu ya taifa ya Misri inashika nafasi ya kwanza kwa timu yenye umri mkubwa zaidi kwenye michuano ya mwaka huu ikiwa na wastani wa umri wa miaka 28.67 ikifuatiwa na taifa la Cape Verde.

Makala Nyingine

More in AFCON