Connect with us

AFCON

SADIO MANE AITAJA AFCON HII KUWA NI NGUMU.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane amesema michuano hii ya AFCON 2023 itakuwa ni migumu kulinganisha na iliyopita kwa sababu nchi zote kubwa zimefuzu.

Mane amezungumza hayo kuelekea mashindano ya AFCON 2023 yatakayoanza Januari 13, ambapo Senegal wapo kundi C na timu za Cameroon, Guinea na Gambia.

“Tunajua haitakuwa rahisi lakini tutakuwepo pale kuonesha ubora wetu na kujaribu kupita kila hatua. Tunatarajia mashindano magumu”.

“Mashindano haya yatakuwa moja ya mashindano magumu tangu nimeanza kuyacheza kwa sababu nchi zote kubwa zipo na wote wana malengo yao, lakini tutaona nini kitakachotokea”.

—Amesema Mane.

Mane alipoulizwa itakuwa na maana gani kwake endapo atashinda kombe hili kwa mara ya pili mfululizo alijibu :

“Kwanza, kushinda AFCON ilikuwa ni kombe bora nimewahi kushinda kwenye maisha yangu na kuja kushinda tena itakuwa kitu cha kipekee na mafanikio makubwa”.

“Imekuwa ni ndoto kucheza katika mashindano haya tangu nilipokuwa mtoto na tutafanya kila lililo bora”.

“Kushinda AFCON itakuwa na matokeo makubwa kwa soka letu kwa sababu (Senegal) tumeshinda kwenye nyanja zote ambapo ni kitu kizuri kwa nchi”.

  • Sadio Mane aliongeza.

Michuano ya AFCON 2023 itaanza rasmi kurindima January, 13, 2024 nchini Ivory Coast na bingwa mtetezi ni timu ya Taifa ya Senegal.

Makala Nyingine

More in AFCON