Connect with us

Taifa Stars

MORRISON ANA NDOTO ZA KUITUMIKIA TAIFA STARS.

Nyota Bernard Morisson ameweka wazi kuwa bado ombi lake la kuomba uraia wa Tanzania lipo palepale na amekiri kufanya mawasiliano Mara kadhaa na Naibu Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Hamis Mwinjuma (mwana FA) juu ya ombi hilo.

Morisson ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Simba na Young Africans kwa nyakati tofauti aliyasema hayo katika mahojiano na Nick Reynold maarufu Bongo Zozo ambaye alimtembela nyumbani kwao Takoradi nchini Ghana.

Mara kadhaa kabla hajaondoka Tanzania Morisson alikuwa akiweka wazi matamanio yake ya kupata uraia wa Tanzania siku moja na kuiwakilisha timu ya taifa ya Tanzania kwenye michezo ya mashindano mbalimbali.

Kwa sasa anaitumikia klabu AS FAR Rabat ya Morocco lakini wakati huu yupo kwao Takoradi nchini Ghana akiuguza majeraha ambayo yalipelekea kufanyiwa upasuaji.

Makala Nyingine

More in Taifa Stars