Leo michuano ya kombe la mapinduzi inaendelea kwa michezo miwili ya hatua ya robo fainali, Yanga itashuka dimbani kuikabili APR majira ya saa 2:15 usiku.
Huku Mlandege na KVZ zikichapana majira ya saa 10:15 Jioni kwenye uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.
Hizi ni baadhi ya takwimu za michuano hii hatua ya makundi.
- Hadi hivi sasa jumla ya magoli 40 yamefungwa kwenye michuano hii.
- Ni timu mbili zilizofunga magoli mengi zaidi hadi hivi sasa [7] klabu za Yanga na Singida Fountain Gate.
- Yanga ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi [5-0] kwenye mchezo mmoja kuliko timu yoyote ile.
- Jamhuri ya Pemba ndio timu pekee iliyofungwa magoli mengi zaidi [5-0] kwenye mchezo mmoja kuliko timu yoyote kwenye mashindano.
- Klabu za JKU na Jamhuri ya Pemba ndio timu zilizoruhusu magoli mengi zaidi hadi hivi sasa kwenye mashindano haya [8].
- Klabu ya Chipukizi ndio timu pekee iliyifunga magoli machache zaidi kwenye michuano hii [1].
- Klabu ya JKU imemaliza michuano bila ushindi wala sare, imepoteza mechi zote tatu [3] za hatua ya makundi.
- Yanga, Simba, Azam na KVZ ndio klabu zilizofungwa magoli machache hadi hivi sasa [1] kuliko timu zingine.
- Kwenye michezo 18 ya hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi , mshambuliaji wa Azam FC Alassane Diao ndiye kinara wa kuibuka mchezaji bora wa mechi akifanya hivyo mara mbili (2) kwenye mechi za tatu za kundi lao .
Wachezaji wengine walioibuka wachezaji bora wameshindwa kuwa na muendelezo kwenye michezo iliyofuata
- Simba vs APR
Hussein Abel (GK)
- Jamhuri vs Jamus
Abdillah Ramadhani
- Yanga vs KVZ
Athuman Salum
- Mlandege vs Chipkizi
Sleiman Said (GK)
- Simba vs Singida
Fabrice Ngoma
- APR vs JKU
Ramadan Niyibizi
- Jamus vs Yanga
Benjamin Laku
- Vital vs Azam
Alassane Diao
- JKU vs Simba
Fondoh Che Malone
- Singida vs APR
Eldin Shaiboub
- Jamhuri vs Yanga
Crispin Ngushi
- KVZ vs Jamus
Omer Michael
- Chipukizi vs Azam
Alassane Diao
- Mlandege vs Vital O
Abdallah Yassin
- JKU vs Singida
Elvis Rupia
- KVZ vs Jamhuri
Akram Mhina
- Vital vs Chipkizi
Suleiman Said
- Mlandege vs Azam
Yannick Bangala.