Connect with us

AFCON

ADEL AAHIDI KUWAONDOA KIKOSINI MASTAA.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Adel Amrouche ameweka wazi kuwa baadhi ya wachezaji aliowajumuisha kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 27 hawajaonyesha uwezo ule aliokuwa anautaka kwenye mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya Misri uliomalizika kwa kichapo cha goli 2-0.

Adel Amrouche amesema kama wataendelea kucheza chini ya kiwango alichokitarajia basi atawarudisha nyumbani na kujumuisha wengine.

“Najua kile tulichonacho, kama unashillingi mia mbili [200 TZS] hauwezi kusafiri kutoka hapa na kigoma, lazima uwe mkweli, kuna baadhi ya wachezaji kile wanachokitoa sio kile ninachokifikiria”.

“Unajua huo ndio ukweli na tumeona, hatuhitaji majina, tunahitaji wachezaji ambao wanaweza kufanya kitu”.

“Nimefurahishwa na baadhi ya wachezaji lakini wengine hawajanifurahisha, na wanajua hatuna muda wa kutosha wa kuwarekebisha wote”.

“Nimefurahishwa na urejeo wa Tshabalala [Mohamed Hussein Zimbwe], Tarryn na Charles kama kawaida, unajua kuna baadhi ya wachezaji wanajitoa sana, lakini kuna watu ambao kama hawatabadilika sasa hivi nitawarudisha nyumbani huo ndio ukweli”.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kimesafiri hii leo kuelekea nchini Ivory Coast tayari kwaajili ya michuano mikubwa ya Afrika [AFCON 2023].

Hii ni makala ya tatu [3] kwa upande wa Tanzania kushiriki michuano hii ya AFCON.

Makala Nyingine

More in AFCON