Connect with us

Boxing

MWAKINYO SIO HADHI YANGU – MFAUME MFAUME

Bondia Mfaume Mfaume amesema kuwa alikataa kushiriki kama Bondia Mshiriki kwenye pambano la Hassan Mwakinyo la “Mtata Mtatuzi” kwakuwa asingeweza kupigana kama pambano la pili halafu pambano kuu liwe la Mwakinyo.

Kwa heshima ya Naccoz itakuwa tumejidhalilisha sana kwakuwa huyo bondia anayepigana pambano kuu sio wa hadhi yangu. Mimi nina mashabiki wengi na napendwa sana, Sasa haiwezekani mimi nipigane halafu mara niondoke ukumbi ubakie mtupu. Halafu huyo bondia wao ndio apigane pambano kuu, labda promota angeweka mzigo mkubwa sana nikimaliza nashusha hata ghorofa.

Katika upande mwingine bondia huyo amesema kuwa yeye hapendi Kummzungumzia sana Hassan Mwakinyo kwakuwa sio bondia profesheno.

Mabondia wapo wengi sana ambao ni mapro, Twaha(Kiduku), Ibrah(Class), Galiatano(Ismail), Kidunda(Selemani) lakini sio huyo mtoto wa Tanga. Yeye sio bondia profesheno, yeye hachezi ngumi anapigana tu na maneno mengi. Mimi siwezi kupigana na bondia kama huyo.

Alipoulizwa kuhusu mahusiano ya mabondia alijibu kuwa

Mabondia takribani asilimia 99 tuna mahusiano mazuri sana na kushirikiana katika mambo mengi tu. Kasoro huyo mmoja tu ambaye mi namuona ni mbinafsi tu.

Aidha Mfaume hakuacha kuzungumzia mipango yake ya mwaka huu.

Ujue mwaka 2023 nilipigana pambano 1 tu pekee kutokana na changamoto za hapa na pale ikiwemo maradhi ya mikono zilizonifika lakini mwaka huu niko fiti sana na huu ni mwaka wangu wa kupigana na yoyote yule atakaye ilimradi promota afike dau zuri tu. Nina mpango mwaka 2025 panapo majaaliwa nihamie kwenye Uzito Mkuu wa Kati (Super Middle Weight)

Alimaliza kusema Mfaume Mfaume.

Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni tarehe 27/01/2024 kwenye usiku uliopewa jina la “MATATA MTATUZI” atakapomenyana na Bondia Mbiya “Hammershock” Kanku kutoka nchini DR Congo kwenye pambano la Raundi 10, Uzito wa Kati(Middle Weight).

Pambano hili la Mkanda wa WBO litafanyika kwenye Ukumbi wa ndani wa NEW AMAAN COMPLEX.

Makala Nyingine

More in Boxing