Connect with us

AFCON

NIGERIA YAPATA PIGO JINGINE TENA KUELEKEA AFCON 2023.

Mshambuliaji kinara wa klabu ya Bayer Leverkusen na timu ya Taifa ya Nigeria Victor Boniface anatarajiwa kukosekana kwenye fainali za mataifa ya Afrika baada ya kupata jeraha la nyonga [Groin Injury] wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Nigeria dhidi ya Guinea.

Kwenye mchezo huo licha ya kuwa na washambuliaji tishio Duniani kwasasa Nigeria ilipoteza kwa jumla ya magoli mawili [2-0] mbele ya Guinea.

Huu ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa kirafiki wa Nigeria kabla ya kuianza safari ya kuelekea nchini Ivory Coast kwaajili ya michuano ya fainali za mataifa ya Afrika [AFCON 2023] zinazoanza kutimua vumbi January 13 mwaka huu.

Sasa Victor Boniface atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita [6] akiuguza jeraha lake, hili ni pigo jingine kwa timu ya Taifa ya Nigeria baada ya siku kadhaa kumkosa kiungo wake tegemezi Wilfred Ndidi aliyeumia wakati akiitumikia klabu yake ya Leicester City siku chache kabla ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa.

Makala Nyingine

More in AFCON