Connect with us

AFCON

MABINGWA AFCON WAITEMBELEA TIMU YA TAIFA KUIPA HAMASA.

Timu ya Taifa ya Ghana wakati ikifanya mazoezi yake jana Jumamosi ilitembelewa na magwiji wa soka la nchi hiyo waliowahi kutwaa taji la mataifa ya Afrika wakiwa na kikosi hicho.

Magwiji hao ni Rev. Osei Kofi aliyewahi kuwa mfungaji bora wa mashindano ya Mataifa ya Africa [AFCON 1965] yaliyofanyika nchini Tunisia.

Mlinzi wa zamani wa Ghana James Kuuku Dadzie, huyu anatambulika kama mlinzi bora zaidi wa kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kuwahi kutokea. [Bingwa AFCON 1978]

Kofi Pare, mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana ambaye alisifika kwa upachikaji mabao zaidi kwenye klabu zake alizocheza na timu ya Taifa akiifungia magoli 15 pekee, anashikiria rekodi ya kufunga goli 6 peke yake kwenye mechi moja. [Bingwa AFCON 1965]

Willie klutse, huyu ni mshambuliaji aliyekuwa kwenye kikosi kilichobeba ubingwa wa AFCON 1978, michuano iliyofanyika nchini Ghana huku akifunga goli katika mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria.

Nyota huyu alichaguliwa kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Guinea, mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia 1978 lakini hakutokea kwenye siku ya mchezo.

Ghana kwasasa ipo kundi B ikiwa na timu kama Misri, Cape Verde na Msumbiji, hadi hivi sasa ina alama moja pekee na ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi B.

Lengo kubwa la nyota hao kufika uwanja wa mazoezi wa BengerVille jana Jumamosi ni kuwapa hamasa wachezaji kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji utakaopigwa kesho Jumatatu.

Makala Nyingine

More in AFCON