Connect with us

AFCON

SAMATTA: MIMI NA MSUVA TUNAJUANA VIZURI.

Mshambuliaji wa klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta jana aliyoa pasi ya mwisho kwenye goli alilofunga Simon Msuva kwa upande wa Tanzania kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Zambia.

Nahodha Mbwana Ally Samatta amesema kucheza kwa pamoja na Simon Msuva kwa muda mrefu kwenye timu ya Taifa kumesababisha kujuana zaidi.

“Ni mchezaji ambaye tumekuwa naye kwa muda mrefu kwenye kikosi cha timu ya Taifa, mara nyingi anajua ninapokuwa na mpira ni nini anatakiwa kukifanya, na mimi nafahamu aina yake ya uchezaji na wapi naweza kumpa mpira akafanya vizuri”.

“Kuwa pamoja kwa muda mrefu kuna tusaidia kufahamu, kujuana na kuweza kusaidia katika mchezo”, Alisema Samatta.

Mchezo unaofuata kwenye hatua ya makundi itakuwa dhidi ya DR Congo, kama Tanzania itashinda mchezo ujao basi itafuzu hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza.

Makala Nyingine

More in AFCON