Connect with us

AFCON

KOCHA STARS: MCHEZO WA KESHO NI FAINALI KWETU.

Kaimu kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Suleiman ameweka wazi kuwa mechi ya kesho dhidi ya DR Congo itakuwa fainali kwa upande wao.

Hemed amesema kutokana na umhimu huo, kikosi chake kitashambulia wakati wote ili waondoke na alama zote tofauti na kilichotokea kwenye mchezo dhidi ya Zambia.

“Maandalizi yapo vizuri baada ya kumaliza mechi na Zambia, tupo vizuri na tupo tayari kupambana na Congo DR”.

“Tunacheza fainali kesho, tunahitaji kupata ushindi na nafikiri mechi ya kesho tutashambulia”, Kocha wa Stars Hemed Morocco.

Nahodha wa kikosi cha Taifa Stars Mbwana Ally Samatta ameweka wazi kuwa makosa waliyoyafanywa kwenye mchezo wao dhidi ya Zambia hayatajirudia tena.

Huku akisisitiza kuwa kila mchezaji amejiandaa vyema kwaajili ya mchezo huo na wanaimani watashinda na kusonga mbele kwenye michuano hii.

“Kama tuliamini tunaweza kupata ushindi na Zambia, basi hivyo hivho kwenye mechi na Congo”.

” Kwa upande wa wachezaji wote wanaelewa umhimu wa mchezo wa kesho na nini wanachotakiwa kukifanya, tutaenda kupambana kuhakikisha tunapata ushindi”, Mbwana Ally Samatta, Nahodha, Taifa Stars.

Tanzania itakuwa na kibarua kesho saa tano [23:00] usiku dhidi ya Congo DR na mshindi wa mchezo huo ana nafasi ya kufuzu kwenda hatua ya 16 bora ya AFCON 2023.

Makala Nyingine

More in AFCON