Connect with us

Makala Nyingine

MOROCCO NA CONGO DR KUCHUNGUZWA NA CAF.

Shirikisho la soka Barani Afrika limeanza kufanya uchunguzi juu ya tukio la vurugu lililofanyika kwenye mchezo wa kundi F kati ya Morocco dhidi ya DR Congo.

CAF itafanya uchunguzi kwa mashirikisho yote mawili kwa maana ya lile la Morocco [FMRF] na lile la Congo DR [FECOFA], mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Taarifa kutoka shirikisho la soka Barani Afrika zinasema kuwa maamuzi na hatua zaidi zitawekwa wazi baada ya uchunguzi kukamilika.

Congo DR na Morocco zipo kundi F sambamba na timu ya Taifa ya Tanzania na Zambia, na timu zote zitacheza michezo yake ya mwisho hapo kesho, Jumatano.

Michezo ya kesho kundi F:

23:00 Zambia vs Morocco
23:00 Tanzania vs Congo DR.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine