Connect with us

AFCON

KOCHA ALGERIA: AFCON HII HAKUNA TIMU KIBONDE.

Timu ya Taifa ya Algeria imeondoshwa rasmi jana kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast baada ya kumaliza nafasi ya mwisho hatua ya makundi ikiwa na alama moja pekee.

Algeria imekuwa mara ya pili kwao kuburuza mkia kwenye kundi lake wakifanya hivyo kwenye AFCON za mwaka 2021 na msimu huu wa 2023 pia wameburuza mkia.

Algeria walikuwa mabingwa wa AFCON 2019 tangu hapo mambo yamekuwa magumu kwa upande wao kwa misimu miwili mfululizo wakipata matokeo mabaya.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mauritania uliokuwa umebeba matumaini makubwa kwa Algeria kumalizika kwa kichapo cha goli 1-0 alisema kunavitu vimetokea ambavyo hawezi kuvielezea lakini ndio maajabu ya mpira wa miguu.

“Nilichokiona kwenye mchezo huo ni kwamba tumeruhusu goli, tunaweza kurejea tena kulitazama lile goli tulilo ruhusu”.

“Kuna vitu ambavyo siwezi kuvielezea, hatukuweza kufunga licha ya kuwa na mipango na mbinu nzuri”.

“Hayo ndio maajabu ya mpira wa miguu, kama hatuwezi kutengeneza nafasi, kama tulizidiwa kwa nafasi walizotengeneza wapinzani, kama tulipoteza nafasi nyingi, kwahiyo tunaweza kusema kuna sehemu ambayo hatupo vizuri lakini hilo halikuwa tatizo kwenye mchezo tuliocheza kwahiyo ndio vitu ambavyo siwezi kuvieleza”.

“Tumetolewa kwenye mashindano ya AFCON kwa mara ya pili na huo ndio mpira wa miguu, hivyo ndivyo ulivyo”.

“Hatujafanikiwa kufunga na hatukufanikiwa kutengeneza utofauti”.

“Kama nilivyosema hapo mwanzo, hatuna timu ndogo kwenye mashindano haya ya AFCON na unaweza kuadhibiwa muda wowote na mipira ya kutengwa au penati, kwahiyo hatujafanikiwa kumalizia nafasi ambazo tulizitengeneza”, Alisema kocha wa Algeria Djamel Belmadi.

Mabingwa wa AFCON 2019 wameungana na Ghana kuondoka kwenye michuano hii ya AFCON 2023 inayoendelea huko nchini Ivory Coast.

Makala Nyingine

More in AFCON