Connect with us

AFCON

SHAFFIH DAUDA: NAWAPA NAFASI CONGO DR KUSHINDA LEO.

Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajia kutupa karata yake ya mwisho ya hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast dhidi ya Congo DR.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa tano [23:00] usiku wa leo, ukiwa ni mchezo wa kusaka ushindi kwa kila timu ili kupata tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano haya.

Kuelekea katika mchezo huo hakuna mabadiliko makubwa ambayo yanatajwa kufanyika kutoka kwenye kikosi kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya Zambia wakati wakitoa sare ya kufungana goli 1-1.

Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars Hemed Suleiman leo anatarajiwa kumpokea kikosini kiungo wa klabu ya Shakhtar Donetsk Novatus Dismas aliyeukosa mchezo uliopita baada ya kupatiwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco.

Kuelekea katika mchezo huo mwandishi na mchambuzi nguli wa michezo nchini Tanzania, Shaffih Dauda ametoa maoni yake huku akiamini hautakuwa mchezo rahisi kwa Stars.

“Ni mechi ngumu sana kwasababu DRC baada ya kupata point moja kwa Morocco, wanategemea kabisa point tatu mbele ya Tanzania, ili waweze kwenda hatua inayofuata”.

“DRC ni Taifa kubwa, washawahi kuwa mabingwa wa hili kombe, wana wachezaji wenye uwezo mkubwa naamini itakuwa mechi kubwa sana”.

“Congo DR nawapa nafasi kubwa sana ya kupata matokeo, Tanzania bado huwezi ukailinganisha na Congo kwa maana ya uwezo, kama ikitokea matokeo Tanzania ameshinda nitafurahi Kama Mtanzania”, Amesema Shaffih Dauda.

Tanzania ina alama moja pekee kwenye kundi ikiwa nafasi ya mwisho, inahitaji alama tatu mhimu hii leo ili iweze kusonga mbele hatua inayofuata na nafasi ipo wazi kwao.

Kocha Hemed Morocco alisema jana kuwa leo wataingia kwa kushambulia zaidi kuliko walivyoingia kwenye mechi zilizopita.

Makala Nyingine

More in AFCON