Connect with us

AFCON

MCHEZAJI MISRI AUMIA KICHWANI AKIPIGA SARAKASI YA MSUVA.

Nyota wa timu ya Taifa ya Misri Emam Ashour hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kitakachoikabili timu ya Taifa ya Congo DR kwenye mchezo wa 16 bora baada ya kupata majeraha ya kichwa akiwa mazoezini.

Emam wakati akiwa mazoezini alifunga goli na kushangilia kwa staili ya kuruka sarakasi badala ya kufikia miguu akafikia kichwa na kuwahishwa hospital kwa matibabu zaidi.

Emam amekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Ivory Coast.

Emam [25] nyota anayekipiga kwenye klabu ya Al Ahly alipatiwa matibabu uwanja wa mazoezi na baadae akakimbizwa hospital kwa matibabu zaidi kwa masaa 24.

Ni pigo jingine kwa timu ya Taifa ya Misri wakati ikijiandaa na harakati za kutwaa ubingwa wa AFCON 2023, mara ya mwisho Misri kutwaa ubingwa ilkuwa mwaka 2010.

Mabingwa mara saba wa AFCON tayari wanamkosa nahodha wao na mhimili mkubwa wa timu hiyo Mohamed Salah pamoja na golikipa wao Mohamed El-Shenawy.

Misri walifanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi lao licha ya kutoa sare katika michezo yake yote mitatu iliyomalizika kwa sare ya magoli 2-2, dhidi ya Msumbiji, Ghana na Cape Verde.

Wapinzani wa Misri, timu ya Taifa ya Congo DR nayo pia haijapata ushindi wowote kwenye kundi lake zaidi ya kutoa sare kwenye mechi zake zote tatu za hatua ya makundi kwenye kundi F.

Congo DR ilitoka sare na Zambia pamoja na Morocco 1-1, na 0-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania.

Makala Nyingine

More in AFCON