Connect with us

Taifa Stars

MZIZE NDIYE MSHAMBULIAJI HATARI KWASASA – UHURU SULEIMANI.

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Uhuru Suleiman Mwambungu amesema kuwa kwenye mashindano ya AFCON msimu huu Taifa Stars ilihitaji zaidi hudumu ya Clement Mzize.

Uhuru ameweka wazi kuwa kwasasa kama Taifa tunapaswa kuendeleza vipaji vya vijana vilivyopo na nyota wa klabu ya Yanga Clement Mzize alistahili kuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichoenda AFCON.

“Tukiachana na ujuaji na upinzani wa ndani, nafikiri nchi inahitajika kushiriki makuzi na maedeleo ya Clemet Mzize”.

“Mzize ndio mshambuliaji hatari kwa sasa tuliyenaye nchini kwetu na hilo limekuwa tatizo kwenye safu ya ushambuliaji kwenye kikosi chetu”.

“sio kwamba hatuna washambuliaji la hasha ila hatuna mshambuliaji hatari mwenye haiba ya mshambuliaji kama Mzize”, aliandika Uhuru Suleiman kwenye ukurasa wa Instagram.

Taifa Stars imefunga goli moja pekee kwenye fainali za mataifa ya Afrika msimu huu katika michezo yote mitatu ya hatua ya makundi.

Stars iliondoshwa ikiwa na alama mbili [2] baada ya kutoka sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

Makala Nyingine

More in Taifa Stars