Kutokana na kauli zake tata na Shutuma kwa timu ya Taifa ya Morocco, Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF) Lilimpa adhabu ya Kifungo cha mechi 8 Kocha huyu huku Shirikisho la soka nchini Tanzania nalo likiamua kumsimamisha kwa muda na kufanya aondolewe kwenye Benchi la Stars na timu kuwa chini ya Hemedi Suleiman Morocco.
DJAMEL BELMADI (ALGERIA)
Kocha huyu anayekunja mkwanja mrefu zaidi kuliko kocha yoyote Barani Afrika(takribani Milioni 550), alitimuliwa punde tu baada ya Timu ya Algeria kufungwa na Mauritania kwa bao 1-0 na kuondolewa kwenye mashindano mapema. Kocha huyo mwenye miaka 47 hajafikia malengo ya Algeria tangua atwae Ubingwa mwaka 2019 hajafanikiwa sio tu kufuzu hatua ya mtoano bali pia kushinda hata mechi 1.
TOM SAINTFIET (THE GAMBIA)
Ndoa tamu kati ya Kocha huyu mwenye miaka 50 na taifa la Gambia imetamatika rasmi baada ya miaka 6 huku Tom mwenyewe akijiuzulu nafasi yake baada ya kushindwa kuivusha timu hiyo hatua ya makundi. Itakumbukwa Tom Saintfiet aliichukua timu hii mwaka 2018 na kuipeleka AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 2021 akiifikisha hatua ya Robo Fainali kumfanya kuwa miongoni mwa makocha Bora Afrika mwaka 2023 lakini ameona imetosha akatafute Changamoto nyingine.
CHRIS HUGHTON (GHANA)
Kuwa kwenye Kundi lenye Timu kama Cape Verde, Mozambique na Egypt, FA ya Ghana haikutarajia lolote lingine zaidi ya taifa lao kufika mbali kwenye michuano hii, lakini kumaliza nafasi ya 3 wakiwa na alama 2 tu pekee wakishindwa kufuzu hata hatua ya makindi ni hali ambayo Uongozi wa soka nchini Ghana ulishindwa kuvumilia na kumtupia virago kocha Chris Hughton huko huko alipo.
JEAN -LOUIS GASSET (IVORY COAST)
Licha ya Kufuzu hatua ya Raundi ya 16 Bora wakiwa kama “Best Looser” Lakini Waandaji hawa na wenyeji wa AFCON 2023 hawajaridhishwa kabisa na mwenendo wa timu yao licha ya kuwa na nyota wengi wakiamini walistahili kufuzu kundi hili bila vikwazo huki wakitandaza Soka safi lakini haikuwa hivyo huku wakipokea kipigo kikubwa kabisa katika historia ya soka la Taifa lao cha mabao 4-0 kutoka kwa Equatorial Guinea. Taarifa za awali zinadai kuwa kuna uwezekano kocha wa zamani wa Taifa hilo na Kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Wanawake ya Ufaransa, Herve Renard kuchukua mikoba hiyo kwa muda, mazungumzo yakiendelea.
JALEL KADRI (TUNISIA)
Tunisia walitoka suluhu ya 0-0 na Afrika Kusini na kuona ndoto zao za kufuzu kuingia hatua ya 2 zikifa na matokeo hayo. Baada ya mchezo huo, kwa mujibu wa BBC, kocha huyo alitangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya kushindwa kutimizia malengo hayo. Tunisia ni miongoni mwa timu zilizotabiriwa kufika mbali kwenye michuano hii lakini Kutoka sare 2 na kufungwa mchezo mmoja kuliwafanya waburuze mkia kwenye kundi hilo la E huku Afrika Kusini, Mali na Namibia wakifuzu.
Nini Kitajiri huko mbeleni kwa makocha waliobakia na hata taarifa za hawa makocha walioachana na Timu zao, baki nasi hapa hapa kwa taarifa zaidi.