Connect with us

EPL

JÜRGEN KLOPP, AHSANTE KWA KUMBUKUMBU.

Uamuzi wa kushtua wa kocha wa klabu ya Liverpool Jürgen Klopp juu ya kuondoka Liverpool ni janga kwa klabu hiyo na mashabiki wake pengo analoliacha linaweza kushindwa kuzibawa kirahisi.

The Reds wanayumba sasa baada ya bosi wao mwenye mvuto kutangaza kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu

Jurgen Klopp amezungumza kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu kama meneja wa Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

Ninaweza kuelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu lakini tayari nimekwisha fanya maamuzi.

Alisema Jûrgen Klopp kocha wa Liverpool.

Huenda hiyo ni kauli duni ya karne hii.

Tangazo la Ijumaa asubuhi limeshangaza ulimwengu mzima wa soka. Hakuna mtu aliyeona hili likitokea hivi karibuni.

Licha ya kurekebisha safu yao yote ya kiungo msimu uliopita wa joto, Liverpool wako kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza na bado wako kwenye kinyang’anyiro cha kushinda vikombe vitatu.

Ndio ni maamuzi magumu sababu nahisi kuishiwa nguvu ya kuhudumu hapa.

Alisisitiza kocha wa Liverpool Jürgen Klopp.

Na hilo linaeleweka, ikizingatiwa ni kiasi gani amewekeza kwenye klabu hiyo tangu achukue nafasi hiyo mwaka 2015.

KLOPP ALITAKA TU KUWAFURAHISHA MASHABIKI WA LIVERPOOL.

Upendo wake kwa Liverpool ni wa kweli sana; imekuwa dhahiri tangu alipowasili Anfield. Yeye aliweza kuendana na ukubwa na tamaduni bora zaidi za timu hiyo, amekuwa akitaka tu kuwafurahisha watu, haswa mashabiki wa klabu ya Liverpool.

Kwa hiyo, haishangazi hata kidogo kwamba amechoka, kwamba maadili yake ya kazi yamemletea madhara makubwa.

Pia hakuna ubishi kwamba kulikuwa na nyakati msimu uliopita ambapo alionekana amechoka. Matokeo hayakuwa yakienda sawa kwa upande wake na matokeo yasiyo ya kuridhisha yaliyopelekea kuzuka kwa maswali mengi juu ya kikosi chake.

Katikati ya haya yote, ilielezwa kuwa hajawahi kuhudumu kwenye timu moja miaka saba katika vilabu vyake viwili vya awali nchini Ujerumani, na kusababisha mazungumzo kuwa historia ilikuwa ikijirudia Merseyside.

KUAMSHA KUMBUKUMBU ZA ‘MABINGWA WA KILA KITU’

Hata hivyo, Klopp alionekana kufurahishwa na kutiwa nguvu tena tangu arejee kutoka kwenye maandalizi ya msimu, akionekana kufurahia kazi ya kuirejesha Liverpool kwenye hali yake baada ya kushindwa kuchukua ubingwa msimu uliopita na kujaribu tena kwenye msimu huu wa 2023-24.

Matumaini yake mapya na imani yake imeonyeshwa katika utendaji mzuri wa timu yake, zimekuwa zikiibua kumbukumbu za ‘mabingwa wa kila kitu’.

Na ni pande ngapi katika historia ambazo zimewahi kumuwakilisha vyema kocha uwanjani? Katika ubora wao, Liverpool ya Klopp ni yenye bidii, yenye shauku na wasiochoka kabisa.

MATATIZO NYUMA YA PAZIA?.

Ndio maana uamuzi huu unashangaza sana. Klopp ameonekana kama mtu wake wa zamani msimu huu. Hakujawa na dalili za uchovu au kufadhaika.

Bila shaka, kutakuwa na uvumi kwamba kuna mengi ya kuondoka kwake karibu kuliko uchovu. Bila shaka kutakuwa na mazungumzo ya kutoridhika nyuma ya pazia.

Watu kadhaa wakuu wamejiondoa katika klabu hiyo kwa miaka kadhaa iliyopita na kumekuwa na gumzo la mara kwa mara kuhusu madai ya Fenway Sports Group kusita kumsaidia Klopp katika soko la usajili.

Lakini Klopp anasema kwamba huu ni “ukweli” na kwamba aliachwa bila chaguo ila kuondoka mwishoni mwa msimu. Bila shaka yeye hatatembea peke yake.

SHUJAA WA LIVEPOOL.

Klopp atashuka kama mmoja wa makocha wakubwa katika historia ya klabu, gwiji wa kweli wa Liverpool. Alichukua klabu katika mkanganyiko mkubwa na kuibadilisha kuwa moja ya timu bora zaidi duniani na bila msaada wa serikali.

Kwa kweli, kulikuwa na matumizi makubwa ya pesa lakini Klopp alifanya maajabu na karibu kila mchezaji aliyefika kwenye timu hiyo alionesha kuivujia jasho jezi ya Liverpool.

Lakini kulikuwa na zaidi ya hilo. Anfield ilimpenda Klopp kwa sababu ya tabia yake na mashabiki watakuwa na deni kwa na kuvutiwa na meneja mwenye mvuto wa kejeli ambaye ujuzi wake wa busara unalingana tu na joto la utu wake.

UKWELI NI KWAMBA.

Pengo atakaloliacha ni gumu kuzibwa na kuna hofu kwamba kila kitu alichojenga Anfield kitaanguka baada ya kuondoka.

Mashabiki wa upinzani wanajua vyema kwamba Klopp amekuwa chachu ya mafanikio ya Liverpool katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.

SIKU AMBAYO MASHABIKI WA LIVERPOOL WALIKUWA WAKIIOGOPA.

Kwa sababu hiyo hiyo, amepata haki ya kujisalimisha kwa masharti yake.

Anaweza pia kupata mwisho mwema anaostahili. Tayari atacheza mechi ya mwisho katika uwanja wa Taifa wa nchini Uingereza (Wembley) Liverpool ikipangwa kucheza na Chelsea katika fainali ya Kombe la Ligi mwezi ujao.

Lakini wakati mashabiki wa Liverpool wakifurahia nafasi ya kutoa shukrani zao kwa Klopp, watakuwa pia na wasiwasi sana hivi sasa juu ya kile kitakachofuata.

Bila shaka hakuna atakayedumu kwenye timu moja milele, alikuwepo Sir Alex Ferguson na Manchester yake, Arsene Wenger na Arsenal yake. Klopp alisema kuwa Liverpool na mashabiki wake watapitia hali hii na leo wanapitia hali hii. Siku hii ya kutisha daima itakuja na hatimaye imewadia.

Ni kwamba hakuna mtu aliyefikiria kwamba siku hii ingefika hivi karibuni. Hili si jambo la kushtua tu kwa wafuasi wa Liverpool; bali ni janga.


Makala Nyingine

More in EPL