Connect with us

AFCON

DJEMBA: BINGWA AFCON ATATOKA TAIFA DOGO KISOKA.

Nyota wa Zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon Eric Djemba Djemba ameweka wazi kuwa mashindano ya mwaka huu ya AFCON ni magumu sana kutokana na timu ambazo hazikutegemewa kufanya vizuri zimefanya vizuri.

Djemba Djemba anaamini kuwa hakuna timu kubwa itakayolibeba kombe hili bali timu ndogo ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa kwenye mashindano haya.

Eric ameziondoa Morocco, Misri na Senegal kwenye mbio za kulibeba kombe hili la mataifa ya Afrika mwaka huu na kuzipa nafasi Equatorial Guinea, Cape Verde na Afrika Kusini.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United anasema Afrika Kusini inavyocheza ni kama ilivyokuwa inacheza Cameroon ya miaka 10 iliyopita.

“Nina uhakika timu moja ndogo kati ya hizi zilizoingia 16 bora itabeba kombe la Mataifa ya Afrika msimu huu”.

“Hautaiona Senegal ikibeba ubingwa huu, hautaiona Morocco wala Misri ikibeba kombe hili, hazipo kama Cameroon ya miaka ya nyuma, ninapoziona zinacheza natamani hadi kulia”.

“Kuna timu tatu ambazo zinapambana kwaajili ya kulibeba kombe hili, Equatorial Guinea, Cape Verde na Afrika Kusini”.

“Timu zote tatu zinaonekana kuwa vizuri, ukiiona Afrika kusini inacheza ni kama Cameroon ya miaka kumi [10] iliyopita”.

“Nina uhakika bingwa atatokea kwenye hizi nchi ndogo kimpira”, Alisema Eric Djemba Djemba.

Makala Nyingine

More in AFCON