Connect with us

Taifa Stars

MASHUJAA TAIFA STARS WAMEREJEA NCHINI.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kimerejea nchini kikitokea nchini Ivory Coast ambapo kilikuwa kinashiriki fainali za mataifa ya Afrika [AFCON 2023].

Hiki ndio kikosi kilichofanya vizuri zaidi kwenye fainali hizi za AFCON ukilinganisha na kikosi kilichoshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza na mara ya pili.

Kikosi kilichoipeleka Stars kwenye makala ya kwanza kiliambulia alama moja [1] na magoli matatu [3], Kikosi cha pili [2019] kiliambulia goli mbili [2] na alama [0].

Kikosi hiki kimebeba alama mbili [2] na kimefunga goli moja [1] peke.

Kipee kabisa timu zote tatu zilizoshiriki AFCON zilimaliza nafasi ya mwisho ya makundi ambayo zilipangwa.

Haya ni maendeleo makubwa ya soka la Tanzania, na wadau wengi wanaamini kikosi hiki kinapaswa kuendelezwa na sio kuvunjwa ili siku moja kilete furaha ambayo watanzania wote wanahitaji.

Makala Nyingine

More in Taifa Stars