Cape Verde itamenyana na Mauritania katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny siku ya Jumatatu (leo) jioni.
Cape Verde iliongoza kundi lao kwa ushindi dhidi ya Ghana na Msumbiji, na kutoka sare na Misri.
Mauritania, iliyo nafasi ya tatu ya kufuzu, ilipata ushindi dhidi ya Algeria. Cape Verde iko katika kiwango bora sana, kitakacho pelekea iwe changamoto kwa Mauritania.
TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA CAPE VERDE.
Bebe amekosekana kwenye kikosi cha washindi wa Kundi B tangu kupata majeraha katika ushindi dhidi ya Msumbiji. Haijulikani ikiwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United atapatikana katika mchezo wa leo.
Kikosi cha Abdou kinaweza kumtegemea Aboubakary Koita, mshambuliaji hatari, mwenye kasi, nguvu na uwezo wa kupiga chenga.
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA CAPE VERDE KINACHOTAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA MAURITANIA:
TAARIFA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MAURITANIA.
Mohamed Dellahi Yali, mfungaji mabao mazuri dhidi ya Algeria, hana uhakika wa kucheza mchezo wa leo kutokana na jeraha alilopata katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Fennecs.
Hata hivyo, wakiwa na kikosi kilichokamilika wanatazamiwa kuishangaza Afrika kwa kutinga katika hatua ya robo fainali kama ambavyo safari yao ilivyokuwa kuanzia hatua ya makundi.
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA MAURITANIA KINACHO TAZAMIWA KUANZA DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA CAPE VERDE.
Timu za mataifa haya mawili zimekutana mara mbili katika michuano hii ya Mataifa Barani Afrika.
Takwimu zikionesha Mauritania amekuwa mbabe kwa Cape Verde kwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja. Huku timu ya Taifa ya Mauritania ikifanikiwa kuzifumania nyavu za Cape Verde mara mbili (02) dhidi ya moja (01) ya Cape Verde.